Tuesday, April 16, 2013

MAREKANI YASHAMBULIWA KWA MABOMU-WATATU WAFARIKI NA MAMIA KUJERUHIWA

marathon



boston marathon explosions first responders

first responders boston marathon

first responders boston marathon

first responders boston marathon


BOSTON-MAREKANI,
Uchunguzi unaendelea kuwasaka watu waliohusika na mashambulizi mawili ya mabomu mjini Boston nchini Marekani wakati wa mbio ndefu na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo yalitokea katika mstari wa kutamatisha mbio hizo, saa kadhaa baada ya washindi kupatikana katika mbio hizo ndefu wakati  wanariadha wengine wakiendelea kukimbia .
Shirika la FBI linaoongoza uchunguzi huo wa mashambulizi  hayo ambayo yanashukiwa kuwa wa kigaidi, uchunguzi ambao unalenga kufahamu kiini cha mashambulizi hayo na waliyoyatekeleza.
Polisi wanasema kuwa watu 17 wamejeruhiwa vibaya huku wengine wakikatwa miguu na mikono kutokana na uzito wa majereha yao.
Rais wa Marekani Barrack Obama amesema kuwa lazima waliotekeleza mashambulizi hayo wachukuliwe hatua za kisheria, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akilaani tukio hilo.
Shambulizi la kwanza lilitokea saa mbili baada ya washindi kuvuka mstari wa mwisho huku polisi wakiwa na wakati mgumu kuwasaidia wale waliokumbwa na milipuko hiyo.
Polisi mjini Boston wametoa wito kwa wakaazi wa mji huo kuepuka mikusanyiko ya watu wakati huu ambao bado hali ya usalama si ya kuridhisha kutokana na mashambulizi hayo.
Miaka kumi iliyopita mashambulizi ya mabomu yalisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tatu  mjini New York,Washington DC  na Pennsylvania.

No comments:

Post a Comment