Mitt Romney Akiwa Jerusalem. |
Marekani,
Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican Mitt Romney ametibua tena anga za kimataifa baada ya kutoa matamshi yenye kuwakwaza Wapalestinakatika kampeni zake na ziara zake huko Israel. Mitt Romney ambaye hivi karibuni aliwatibua waingereza kwa kauli yake ya kuwa na wasiwasi kama Uingereza ipo tayari kwa michuano ya Olympic, ametamka kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa Israel kitu ambacho hakitambuliwi na Wapalestina na washirika wake.
Pia Romney amesema katika ushindani wa kiuchumi kati ya Israel na Palestina ni Israel ndiyo iliyotajiri zaidi kutokana na utamaduni wake ambao ni bora zaidi ya Palestina.
Mpatanishi wa mgogoro wa Israel na Palestina kutoka Palestina Saeb Erekat amesema maneno hayo ya Romney yalikuwa ni ya kibaguzi sana akiyataja kama 'matamshi ya kibaguzi yanayoonesha ukosefu wa maarifa'."Kila mmoja anajua Palestina haiwezi kufikia ustawi wake kwa kiwango cha juu chini ya vizuizi vya Israel" Aliongeza Bw.Saeb.