Thursday, November 29, 2012

KILI STARS YAFUNGWA NA BURUNDI

UGANDA,
Timu za soka Tanzania, Kilimanjaro Stars na Timu ya Taifa ya Burundi zimekabiliana vikali na katika mchezo wa pili wa leo kwenye mashindano ya Chalenji CECAFA katika uwanja wa Namboole nchini Uganda.
Matokeo ya mchezo huo Burundi imeibamiza Kilimanjaro Stars kwa bao 1-0 kupitia bao lililofungwa kwa njia ya penati katika kipindi cha pili.http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2011/11/Kilimanjaro-Stars.jpg?width=650


Matokeo hayo yanaiweka Kilimanjaro katika shinikizo la kushinda mchezo wake na Somalia kwa magoli mengi ili waweze kusonga mbele.
Katika mchezo wa awali Somalia imeondolewa katika mashindano ya mwaka huu ya soka kuwa ni taji la Afrika Mashariki na kati CECAFA inayoendelea jijini Kampala Uganda.
Sudan walipata bao lao la ushindi katika dakika ya 86 kipindi cha pili kupitia mchezaji Mohammed Farid baada ya vijana hao kujaribu kutafuta bao la mapema bila ya mafanikio.
Ikilinganishwa na mchuano wa kwanza dhidi ya Burundi walikofungwa mabao 5 kwa 1,Somalia ilicheza mchezo wa hali ya juu huku ikishika kiwango cha kati na pia kushambulia lango la Sudan lakini umaliziaji haukuwa mzuri.
Kocha wa Somalia Mganda Sam Ssimbwa alikuwa amesema hapo awali kuwa alitarajia kikosi chake kingefika katika awamu ya nusu fainali baad aya kukinoa kikosi hicho kwa wiki mbili.
Sudan nayo ilianza mchuano wao wa ufunguzi kwa kusuasua baad aya kuchanagwa na Tanzania kwa mabao mawili kwa bila.
 

No comments:

Post a Comment