Thursday, November 1, 2012

YANGA YAIFUATA SIMBA KILELENI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh1-Xz2FF3S74puVk0p_AN0lYvK0cKtRTvYbJge0CDeIHHNLavDinu0JjY0Kfwwt42d4rvrsVP6WJjDQbfBy8aPuc8jsPK_oeKGKrAFW-rQZOcfZ_LS-NN6QTOZbaOmHlnkkosAxi-0hk/s640/DSC_5634.JPGDAR ES SALAAM-TANZANIA,
TIMU ya Yanga leo imeichapa Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huu, unaifanya Yanga iwe na pointi sawa na mabingwa watetezi, Simba SC waliotoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro uwanja wa Jamhuri

Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa  na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier Kavumbangu.

Cannavaro alifunga kwa kichwa krosi ya Oscar Joshua dakika ya pili, wakati Kavumbangu alimalizia pasi ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.

Kipindi cha pili, Yanga walirudi na moto wao tena na kuendelea kuliandama lango la Mgambo JKT na Yanga dakika 34 kupata bao la tatu, mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Kavumbangu.

Mgambo JKT ilipata pigo dakika ya 85, baada ya beki wake wa kulia, Salum Mlima kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu mbaya Mbuyu Twite.

Kikosi cha Yanga; Ally Mustafa ‘Barthez’, Nsajigwa Shadrack, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima.

Mgambo JKT; Godson Mmasa, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum Kipanga, Bakari Mtama, Ramadhani Malima, Chande Magoja, Mussa Ngunda, Issa Kandulu, Fully Maganga na Juma Mwinyimvua

Katika mchezo wa Simba uliochezwa mjini Moro kwenye uwanja wa Jamhuri ilitoka sare ya 1-1 na Polisi na wenyeji wakitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa Mokili Rambo na Amri Kiemba alisawazisha dakika ya 57.

No comments:

Post a Comment