Wednesday, November 7, 2012

NI OBAMA TENA!


MAREKANI,
Rais wa Maerkani Barack Obama ameibuka tena kidedea katika uchaguzi mkali wa kugombea urais wa Marekani,safari hii akimshinda Mitty Romney kwa jumla ya ya kura 303 kwa 206 katika ushindani mkali ambapo Romney alimshinda Obama katika kura za wananchi akipata asilimia 50 dhidi ya 49 za Obama.kaiongea baada ya kutangazwa matokeo rasmi Obama amewashukuru wamarekani kwa kuonesha imani juu ya uongozi wake na kumpa ridhaa y kuongoza tena taifa hilo kwa muhula wa miaka minne ijayo.

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa kushinda rais Obama amesema kuwa kwa sasa anarejea ikulu akiwa na malengo thabiti na mwenye ari zaidi ya awali kwa lengo la kuwatumikia raia wa taifa hilo.
Obama amesema kuwa haijalishi tofauti zozote zilizopo kwa wamarekani bado kwa pamoja inawezekana kulifikisha taifa hilo mbele zaidi katika suala la maendeleo na usalama, ili kuhakikisha ndoto za wamarekani wote zinatimia.

Aidha rais Obama amemshukuru mpinzani wake Mitt Romney kwa kampeni zenye ushindani na kwamba ataendeleza ushirikiano na gavana huyo ili kuliwezesha taifa hilo kusonga mbele kwa manufaa ya wamarekani wote.


No comments:

Post a Comment