Thursday, February 28, 2013

MTANZANIA ATEULIWA KUWA WAZIRI RWANDA.

Profesa Silas Rwakabamba
RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).

Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”

Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.

“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.

Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.

Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.

Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.

Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.(CHANZO:MWANANCHI)

Monday, February 25, 2013

KONDOMU BANDIA ZAUZWA NCHINI

 
DAR ES SALAAM-TANZANIA,
KONDOMU zinazodaiwa kuwa ni bandia ambazo zilipigwa marufuku nchini Uingereza kutokana na kubainika kuwa hazina ubora unaotakiwa, zimetapakaa katika maduka mbalimbali ya dawa nchini, Mwananchi limebaini.
Kondomu hizo ni Durex na Trojan ambazo zina vipele na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa zinauzwa katika maduka mbalimbali ya dawa kwa bei ya Sh5,000.
Mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ya Uingereza ilifanya msako mkali kwa lengo la kukamata mamilioni ya kondomu hizo, wakati ambao ilikuwa imepita takriban miezi 18 tangu zilipokuwa zimeingizwa nchini humo.
Mdhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya wa Uingereza alinukuliwa akisema kuwa mamilioni ya kondomu hizo feki ziliingizwa kutokea Mashariki ya Mbali na kwamba tayari zilikuwa zimetumiwa na idadi kubwa ya watu.
Kondomu hizo zinadaiwa kutokuwa na ubora hali inayoweza kuongeza hatari kwa watumiaji kwa kusambaza kwa kasi magonjwa ya zinaa, virusi vya Ukimwi au kusababisha mimba zisizohitajika, hivyo kuharibu mikakati ya uzazi wa mpango.
Ofisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na gazeti hili jana, alithibitisha kuwapo kwa taarifa za kondomu hizo za Durex na Trojan na kuongeza kuwa mamlaka hiyo imewaagiza wakaguzi wake kuzichunguza ili kubaini kama zina ubora ama la.
“Wakaguzi walichukua sampuli ya kondomu hizo kwa lengo la kuzichunguza, nipe muda kidogo ili nizungumze na mkurugenzi ili kujua uchunguzi ule umefikia wapi,” alisema Simwanza.
Alipotafutwa baadaye alibainisha kwamba uchunguzi wa sampuli hiyo bado upo maabara na kwamba majibu yake hayajatoka. Hata hivyo hakusema ni lini yatatolewa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Leandri Kinabo aliomba apewe muda ili afuatilie kujua ni kondomu za aina gani zilizowahi kukamatwa na kupigwa marufuku zisitumike.
“Nipe muda kidogo nifuatilie ili kujua zilizopigwa marufuku na ambazo tulizizuia kuingizwa nchini, nitafute mchana,” alisema Kinabo ambaye alipotafutwa baadaye alisema yuko kwenye kikao na kwamba alikuwa hajaweza kuwasiliana na watu wa maabara.
Hii siyo mara ya kwanza kuibuliwa kwa taarifa za kuwapo kwa kondomu feki nchini, kwani Desemba 20, mwaka jana kontena lililosheheni kondomu za kiume aina ya Melt Me kutoka nchini India lilikamatwa na kuzuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi.
Maofisa wa TBS walilazimika kufanya msako katika baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuziondoa kondomu hizo katika soko.(MWANANCHI)

RAIS WA KWANZA MWANAMKE AAPISHWA KOREA KUSINI-Apinga mpango wa Nyuklia.

Rais wa Korea kusini, Park Geun-Hye
Rais wa Korea kusini, Park Geun-Hye


Rais wa kwanza mwanamke nchini Korea Kusini Park Geun-Hye ameapishwa leo jijini Seoul katika sherehe iliyohudhuriwa maelfu ya raia wa taifa hilo.

Rais huyo mpya ameahidi kuinua uchumi wa taifa hilo pamoja na kuwaahidi raia wake usalama na kusisitiza kuwa serikali yake haitatishwa na vitisho kutoka kwa jirani zao Korea Kaskazini.
 

Rais huyo pia ameahidi kuhakikisha kuwa ajira zinaundwa nchini humo ili taifa hili liendelee kiuchumi na raia wake kuishi maisha mazuri.
 

Rais Park Geun-Hye mwenye umri wa miaka 61 amekiri kuwa hayo ndio mambo makubwa ambayo raia wake wanatarajia kutoka kwake kama kiongozi wa atatekeleza kama kionhgozi wa nne wa taifa hilo.
 

Park ameitaka serikali ya Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nuklia ili kushirikiana na mataifa mengine duniani .
 

Baba yake Rais Park, mwanjeshi Park Chung-He aliwahi kuongoza taifa hilo kwa miaka 18 miaka hamsini iliyopita kabla ya kuuawa.(RFI)
 

Friday, February 22, 2013

Kanisa katoliki laruhusu tembe za kuzuia mimba

Tembe za kuzuia Ujauzito.


COLOGNE-UJERUMANI,
Kanisa Katoliki nchini Ujerumani limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.

Uamuzi huu umefanywa kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa Katoloki zikisema kuwa kuzima mimba ni kinyume cha maongozi yake.

Mwishowe Maaskofu hao walikubaliana kuwa itakuwa halali ikiwa tembe hizo zitatumiwa na mwanamke aliyebakwa kwa lengo la kuzuia kushika mimba badala ya kutoa mimbaMaaskofu nchini Ujerumani wamekuwa wakijikuta njia panda, ambapo upande mmoja wanahangaishwa na msimamo wa Kanisa Katoliki, na kwa upande mwingine tatizo lililompata mwanamke huyo aliyebakwa, kufukuzwa na hospitali zinazosimamiwa na Kanisa hilo zilizoko mjini Cologne.Hii ina maana kuwa itaweza kutumiwa tu kama kifaa cha kuzuia kushika mimba lakini sio kuavya. Tembe hizo hutumiwa na wanawake wengi wasiotaka kushika mimba baada ya tendo la ndoa.

Hata hivyo Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, ambako Papa wa sasa alitoka, limegawanyika kufuatia tendo hilo la ubakaji.

Ubishi kama huo nchini Marekani haukufikia uamuzi baada ya pande zote zilizokuwa zikibishania dawa hiyo kusema kuwa ni vigumu kujua kama baada ya kitendo cha ndoa asubuhi inayofuata mwanamke ameshika mimba au la.(BBC)

Monday, February 18, 2013

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE) ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
 1.0UTANGULIZI
 Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
 2.0MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1Usajili na Mahudhurio
 Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176
 Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani. 


 2.2Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
 Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihaniwamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
 3.0MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
3.1Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa

(a) Watahiniwa Wote

Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67.  Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012  ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.




(b)Watahiniwa wa Shule

Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50.  Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro,  ugonjwa na vifo.

(c)Watahiniwa wa Kujitegemea

Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 nawavulana 30,084  wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23  hawakufanya mtihani.



4.0MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE



(a) Watahiniwa wa Shule

Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.



(b) Watahiniwa wa Kujitegemea

Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani.  Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361. 





5.0UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.



Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:


8.0TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

8.1           Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.  Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

(i)Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;

(ii)Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na

(iii)Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.

8.2           Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:

(i)Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule.  Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.

(ii) Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.

(iii)Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.

(iv)Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.

(v)Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.



9.0MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA



Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:

(a)           Watahiniwa 28,582wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.

(b) Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.




11.0KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012



(a)Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012  yanapatikana katika tovuti zifuatazo:  

·www.matokeo.necta.go.tz

·www.necta.go.tz   

· www.udsm.edu.ac.tz

· www.moe.go.tz



(b) Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya  ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:



MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA(Mfano:matokeoxS0101x0503)





Dkt.  Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)


WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

MATOKEO YA KDATO CHA NNE -LINK ZINAZOFUNGUKA INGIA HAPA

 http://www.necta.go.tz/img/top_logo.gif


DAR ES SALAAM,-TANZANIA.
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAMETOKA RASMI FUNGUA LINK IFUATAYO INAYOFUNGUKA KWA URAHISI:

LINK YA 2:LINK INAYOFUNGUKA

MAUAJI YA PADRE ZANZIBAR:BARAZA LA MAASKOFU LATOA TAMKO.




http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/02/4834436_orig.jpg





http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/02/999727674.jpg

 http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/02/519118336.jpg
ZANZIBAR-TANZANIA,
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Severin Niwemugizi alisema tukio hilo linatia mashaka kwa kuwa mauaji hayo yanaonyesha kuwa ni ya kupanga.
“Nimepata taarifa kwamba kuna mwenzetu ameuawa huko, lakini inaonekana ni mauaji ya kupangwa kwa kadiri ya hamasa ambazo zinatolewa na dini fulani, kwani waliwahi kusema hatutaifurahia Pasaka, nadhani ndiyo wanatekeleza hilo,” alisema Niwemugizi.
Alisema tukio hilo ni la kuogopesha na linaonyesha nchi inakoelekea si kuzuri kwa kuwa kikundi fulani kimeachiwa na kinafanya mauaji na kuwatendea maovu wengine lakini viongozi wamekaa kimya.
“Hii ni ishara mbaya kwani Serikali ipo hivyo tunahitaji kauli yao kuhusu haya mambo, kwa kweli nina mashaka na yanayotokea ili yasije yakatufikisha kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda,”alisema Niwemugizi.
JK atuma rambirambi
Rais Jakaya Kikwete alisema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Mushi.
“Nimeliagiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”

Sunday, February 17, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUTANGAZWA LEO.

http://70.85.226.211/~tbcgo/images/Philipo%20Mulugo.jpg
Naibu waziri wa Elimu Bw.Philip Mulugo


DAR ES SALAAM-TANZANIA,
Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye matokeo ya kidato cha nne kutangazwa rasmi leo, kwa mujibu wa naibu waziri wa elimu Bw. Philip Mulungo alipokuwa akiongea na Gazeti la Nipashe, amethibitisha kuwa maandalizi yote ya kutolewa matokeo yalikuwa yamekamilika hapo jana na leo Tarehe 18.02.2013 yatatangazwa rasmi.

Padri wa Kikatoliki auawa Zanzibar .

ZANZIBAR-TANZANIA,
http://t1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSw2QWBbKKfbw96OHur67PO3KyNw1YdzT2FkzGMyQJMOzOVbzp6P_05nQWatu waliokuwa na bunduki leo wamempiga risasi na kumuuwa Kasisi wa katoliki Bw. Evarist Mushi ambaye ni Paroko wa Parokia ya Minara Miwili – Zanzibar likiwa ni shambulizi la pili kuwahi kufanywa katika miezi ya karibuni katika kisiwa hicho ambacho idadi kubwa ya wakaazi wake ni Waislamu. Msemaji wa polisi kisiwani humo Mohammed Mhina amesema  alizuiwa na vijana wawili nje ya  lango la kanisa , kabla ya mmoja wao kumpiga risasi kichwani.

 Mhina amesema kwa sasa kiini cha shambulizi hilo hakijajulikana, lakini polisi inafanya msako wa kuwanasa majambazi hao. Mnamo siku ya Krismasi, watu waliokuwa na bunduki  walimpiga risasi na kumjeruhi vibaya kasisi wa kikatoliki wakati akirejea nyumbani kutoka kanisani. 

Haijabainika kama mashambulizi hayo mawili yanahusiana, au  ikiwa yamechochewa na hisia za kidini. Mwezi Novemba mwaka jana, washambuliaji walimmwagia kemikali usoni na kifuani mhubiri mmoja wa kiislamu, na kumekuwa na hofu baina ya jamii hizo mbili kisiwani Unguja.

Tuesday, February 12, 2013

NECTA WATOA TAMKO RASMI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.

Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.

Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi alisema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).

Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.

Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
 
Uvumi huu umetokana na mtu asiyejulikana kufungua akaunti ya facebook yenye jina la Baraza na kuanza kuweka taarifa hizo zisizo sahihi. Napenda kuwajulisha wananchi kuwa Baraza letu halina mtandao kama huo hivyo taarifa hizo si sahihi.

Nchimbi alibainisha kuwa matokeo hayo si siri hivyo yakiwa tayari Katibu Mtendaji atayatangaza kupitia vyombo vya habari na baadaye yataanza kusambazwa kwa kutumia mtandao.

Aliwataka wananchi kuwa makini ili wasitapeliwe na wanaojifanya kuwa wanaweza kupata matokeo ya mwanafunzi kabla hayajatangazwa rasmi kwa vile suala hilo haliwezekani.

CCM YATANGAZA WAJUMBE WAPYA WA KAMATI KUU.

 
 
DODOMA-TANZANIA, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewachagua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri  Kuu Taifa wa chama hicho.

BARA:
 1.Ndg Stephen Masatu Wasirra. 2. Ndg Jerry Silaa. 3. Ndg William Lukuvi.

4.Ndg Alhaj Adam Omari Kimbisa. 5. Ndg Prof Anna Kajumulo Tibaijuka.

6.Ndg Pindi Hazzara Chana. 7. Ndg Emmanuel J Nchimbi.

Wafuatao kura hazikutosha-Bara

-Ndg Chriss Chami, Ndg Said Mtanda, Ndg Mohammed Nyundo,
-Ndg George Mwanisongole, Ndg Michael Lekule Laizer.
-Ndg Dr Fenela Mukangara, Ndg Anthony Dialo, Ndg Raphael Chegeni na wengine.

VISIWANI:

 1.Ndg Dr Salim Ahmed Salim, 2. Ndg Prof Makame Mbarawa.
 3.Ndg Dr Hussein A Mwinyi, 4. Shamsi Vuai Nahodha.
 5.Ndg Dr Maua Abeid Daftari, 6. Ndg Khadija Aboud.
 7.Ndg Samia Suluhu Hassan.

Wafuatao kura hazikutosha- Visiwani

Alli A Karume, Juma Shamhuna, Mohammed Aboud na wengine

Kutokana na uchaguzi huo baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete pamoja na wajumbe kwa kuichagua timu hiyo. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Mtandao wa www.habarimasai.com umeelezwa kwamba wajumbe waliochaguliwa ni makini na kwamba CCM ina imani nao kuwa wataivusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Monday, February 11, 2013

PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUJIUZULU


http://l1.yimg.com/bt/api/res/1.2/OghHOUVGAdw5jkaiqHQlag--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD0zMzM7cT04NTt3PTUxMg--/http://media.zenfs.com/en_us/News/Reuters/2013-02-11T122658Z_1146797572_GM1E92B1JT301_RTRMADP_3_POPE-RESIGNS.JPG

http://l.yimg.com/bt/api/res/1.2/fBMzX47bwjrUut5Sd2DYZQ--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD05MDA7cT03OTt3PTczNg--/http://media.zenfs.com/en_us/News/ap_webfeeds/cef0a2fc2096a524240f6a70670052e7.jpg
 http://l3.yimg.com/bt/api/res/1.2/1bfogd5OFbiezWIzY32kIQ--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD01MDY7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/en_us/News/ap_webfeeds/7bca85b520d8a624240f6a70670087f4.jpg
VATICAN-ITALIA,
Kadinali Joseph Ratzinger ama Papa Benedict XVI  ametangaza uamuzi wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidikutokana na kudhoofu kimwili na kiakili.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.

 Tukio jipya katika karne za hivi karibuni., ambapo papa wa mwisho kujizulu alikuwa ni Papa
Msemaji wa Vatikani Father Federico Lombardi, amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu ya tukio hili.

Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani alipewa ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg, Ujerumani, Georg Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa ameanza kupata shida ya kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya kimaumbile.


VIDEO YA PAPA AKITANGAZA KUJIUZULU:

Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye umri mkubwa wa miaka 78.
Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.

Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa amesema: "baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.

Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki.

Hata hivyo kujiuzulu huko kumepokewa kwa hisia tofauti ambapo wapo waliokubaliana na wengine wakionekana kusita akiwemo katibu mkuu wa Papa John Paul II aliyeshikilia wadhifa wake mpaka mwisho wa uhai wake licha ya kuugua,Kadinali Stanislaw Dziwisz ambaye amewaambia waandishi wa habari nchini Polland kuwa "Haikutakiwa  kushuka kutoka katika msalaba".kwa upande wao viongozi wa duni wameupokea kwa hudhuni uamuzi huo ingawa wameuunga mkono.Waziri mkuu wa Ujerumani  Angela Merkel amesema uamuzi wa papa unapaswa kuheshimiwa ikiwa amejiuzulu kwa kujiona ni dhaifu kutekeleza majukumu yake, huku David Cameron waziri mkuu wa Uingereza akisema Papa benedict XVI atakumbukwa kiroho na mamilioni ya wafuasi wa dini".

FAINALI ZA AFCON-Nigeria Bingwa!-matukio katika Picha.

http://www.mtnfootball.com/live/phase2/photo_admin/Upload/B13BJMN0302w-1360577558.jpg
http://www.mtnfootball.com/live/phase2/photo_admin/Upload/B13BJBA4117w-1360532990.jpg
http://www.mtnfootball.com/live/phase2/photo_admin/Upload/B13BJGB5070w-1360577389.jpg
JJ Okocha ,Kanu wakiwa na kocha Steven Keshi      
http://www.mtnfootball.com/live/phase2/photo_admin/Upload/B13BJBA4294w-1360532990.jpg
Kocha Steven Keshi Shujaa wa Nigeria.
http://www.mtnfootball.com/live/phase2/photo_admin/Upload/B13BJAL1434w-1360533288.jpg
http://www.mtnfootball.com/live/phase2/photo_admin/Upload/B13BJAL1459w-1360533289.jpg

JOHANESBURG-AFRIKA KUSINI,Nigeria wamenyakua kombe la mataifa ya Afrika baada ya miaka 19 baada ya kuwafunga Burkina Faso katika fainali za kombe hilo zilizofanyika uwanja wa taifa huko Johannesburg Afrika kusini.



Nigeria wakicheza kwa mara ya 7 katika fainali hizo walipata gilo la kuongoza katika dakika ya 40 kupitia mchezaji wake maahiri wa kulipwa Sunday Mba, ambapo walifanikiwa kuulinda ushindi huo mpaka mwisho wa mchezo.

ushindi huo umekuwa shangwe kubwa kwa wanigeria na hasa kocha wa timu hiyo Steven Keshi ambaye ameandika rekodi ya kuwa kochawa pili barani Afrika kushinda fainali hizo akiwa kama mchezaji na baadaye kocha.

 Burkina Fasso kwa upande wao licha ya kushindwa watapaswa kujivunia kiwango bora ambacho kimewasaidia kufika fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Sunday, February 10, 2013

Bingwa AFCON 2013, Nigeria au Burkina Faso?

 
 AFRIKA KUSINI,

Mbabe wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, atajulikana leo hii baada ya miamba ya soka barani Afrika, Nigeria na Burkina Faso kupambana katika mchezo wa fainali.
Fainali za mwaka huu zinazofanyika nchini Afrika Kusini, zilishirikisha timu 16, huku mabingwa watetezi wa kombe hilo, Zambia, waking'olewa katika hatua ya makundi.
Timu nane zilisonga hatua ya robo fainali.
Timu hizo ni Afrika Kusini, Burkina Faso, Cape Verde, Ghana, Ivory Coast, Mali, Nigeria na Togo.
Nigeria ambayo ilianza kwa kusuasua katika hatua ya makundi, imeonyesha mchezo mzuri katika mechi zake zilizofuata kuanzia ngazi ya robo na nusu fainali.
Ikicheza hatua ya robo fainali, Nigeria iliifunga Ivory Coast mabao 2-1, huku Ghana ikiifunga Cape Verde mabao 2-0.
Baada ya kutinga nusu fainali, Nigeria iliiadhibu Mali magoli 4-1. Nayo Burkina Faso ikishinda magoli 3-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 dakika 120 za mchezo.