Monday, February 18, 2013

MAUAJI YA PADRE ZANZIBAR:BARAZA LA MAASKOFU LATOA TAMKO.




http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/02/4834436_orig.jpg





http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/02/999727674.jpg

 http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/02/519118336.jpg
ZANZIBAR-TANZANIA,
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Severin Niwemugizi alisema tukio hilo linatia mashaka kwa kuwa mauaji hayo yanaonyesha kuwa ni ya kupanga.
“Nimepata taarifa kwamba kuna mwenzetu ameuawa huko, lakini inaonekana ni mauaji ya kupangwa kwa kadiri ya hamasa ambazo zinatolewa na dini fulani, kwani waliwahi kusema hatutaifurahia Pasaka, nadhani ndiyo wanatekeleza hilo,” alisema Niwemugizi.
Alisema tukio hilo ni la kuogopesha na linaonyesha nchi inakoelekea si kuzuri kwa kuwa kikundi fulani kimeachiwa na kinafanya mauaji na kuwatendea maovu wengine lakini viongozi wamekaa kimya.
“Hii ni ishara mbaya kwani Serikali ipo hivyo tunahitaji kauli yao kuhusu haya mambo, kwa kweli nina mashaka na yanayotokea ili yasije yakatufikisha kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda,”alisema Niwemugizi.
JK atuma rambirambi
Rais Jakaya Kikwete alisema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Mushi.
“Nimeliagiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”

No comments:

Post a Comment