Tuesday, June 5, 2012

MBWANA SAMATA AFUATILIWA NA MAN CITY.

 ABDJAN.IVORY ,COAST
Mpelelezi wa vipaji wa timu ya Manchester City Joe Mulberry  ya Uingereza alikuwepo nchini Ivory Coast kuangalia vipaji vya wachezaji wa Afrika magharibi naKumfuatilia mchezaji wa Taifa Stars anayecheza Nchini Kongo katika klabu ya TP MazembeMbwana Samata.
Mpelelezi huyo alipanga hoteli moja na Taifa Stars na kuangalia mechi yake na Ivory Coast kwa mujibu wa vyanzo vya habari. Ingawa mwanzoni alifanya siri suala hilo baadaye baada ya kubanwa na mwandishi wa habari Edo Kumwembe alikiri na kusema anamchuguza Samata kuangalia maendeleo yake huku akionesha kuwa na rekodi kamili ya mchezaji huyo kutokana kuwa na taarifa lukuki za mchezaji huyo ikiwemo magoli 2 aliyoyafunga katika ligi ya Klabu bingwa Afrika.

Hata Hivyo mpepelezi huyo alisema licha ya Mbwana kuwa mchezaji mzuri bado atahitaji kutafutiwa ligi nyingine za Ulaya kabla ya kucheza ligi kuu ya uingereza ili kukomaa na kuweza kuhimili mikiki mikiki ya ligi hiyo maarufu duniani.




MPELELEZI wa vipaji vya soka toka klabu tajiri England, Manchester City, Joe Mulberry alitua kwa siri mjini Abidjan na kupiga kambi kwenye hoteli ya Ibis Plateau, ambayo pia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilifikia na lengo lilikuwa moja tu kuwachunguza wachezaji wa timu hiyo, Mwananchi limebaini.
Mulberry, raia wa Uingereza mwenye jukumu la kuchunguza vipaji kwa nchi za Afrika Magharibi, alifanya kazi ya kuipeleleza Stars bila kutaka mtu yeyote kufahamu kabla ya mwandishi wa habari hizi kumbaini.
Awali, Mulberry aliyeweka makazi yake nchini Ghana alipanga kwenye chumba namba 604 cha hoteli ya Ibis Plateau.
Baada ya gazeti hili kupata fursa ya kuongea naye muda mrefu, lilimbaini na ndipo naye alipomfichua siri kwamba alikuja Abidjan kwa ajili ya kuangalia pambano la Stars dhidi ya Ivory Coast.
Kwa mujibu wa uchunguzi wake wa haraka, Mulberry alivutiwa na kipaji cha mshambuliaji Mbwana Samata na cha kushangaza katika kipindi kifupi tayari alikuwa amekusanya habari zote za Samata.
Miongoni mwa dodoso muhimu alizokusanya ni pamoja na mabao mawili aliyofunga wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Dynamo ya Zambia na El Merreikh ya Sudan akiwa na timu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mulberry alikiri Samata alikuwa na kipaji kikubwa lakini akataka amuone zaidi siku za usoni kujua kama alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga kama ilivyo katika kuuchezea mpira.
“Nitasafiri kwenda Ghana kumtazama kwa ajili ya pambano la ligi ya mabingwa kati ya Berekum Chelsea dhidi ya TP Mazembe pale Accra, Julai 5. Kama atakuwa yuko safi tena nitajaribu kuzungumza na timu yake.”
Hata hivyo, Mulberry alisema Samata hawezi kucheza katika Ligi Kuu ya England kwa sasa na badala yake anaweza kupelekwa katika ligi nyingine kabla ya kupata uzoefu wa kucheza ligi kubwa Ulaya. 

No comments:

Post a Comment