Saturday, June 30, 2012

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA MISAADA WATEKWA KENYA

Kenya,
Polisi nchini Kenya wameripoti kuuawa kwa raia mmoja wa Kenya na kutekwa nyara kwa wafanyakazi wa sita  wa shirika  la kutoa misaada kwa wakimbizi la Norwegian Refugee Council,(NRC)  katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
 kKambi hiyo inatoa hifadhi kwa wakimbizi nusu milioni na ndiyo inatambulika kama kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.Aliyeuawa ni dereva raia wa Kenya wakati raia waliotekwa ni kutoka Ufilipino, Canada,Norway na Pakistan na wekanya wawili wote wanaume.

Msemaji wa Shirika hilo amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa katibu mkuu Elizabeth Rasmussen alikuwemo kwenye msafara uliovamiwa lakini amenusurika.

Kwa mujibu wa  polisi watu waliokuwa na bunduki walishambulia msafara wa magari katika kambi hiyo na kumuua dereva huyo huku wakiwajeruhi wengine wawili.

Polisi wamehusisha kundi la Al shabaab katika tukio hilo na vyombo vya usalama vimeanza msako mkali ndani ya nchi na kuelekea Somalia kwa mujibu wa Cyrus Oguna msemaji wa jeshi la Kenya.

No comments:

Post a Comment