Friday, June 8, 2012

MOVEMENT FOR CHEANGE (M4C) YA CHADEMA MOTO!

M4C ya Chadema yaendelezwa Mtwara leo

 
Sehemu ya maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara na vitongoji vyake, wakiwasikiliza viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika mkutano wa hadhara wa M4C (Movement For Change), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa. (Picha na Joseph Senga via Francis Dande)

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, akihutubia katika mkutano wa hadhara wa M4C, kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara, leo. (Picha na Joseph Senga via Francis Dande)




 LINDI/MTWARA,
Vuguvugu la  mabadiliko (Movement for change) inayoendelea nchi nzima imeonekana kuvuta usikivu na umati mkubwa wa wananchi ambao wameendelea kujitokeza katika mikutano inayoendeshwa na chama hicho.
Vuguvugu hili ambalo kwa sasa lipo katika mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara limeonekana kuvuta idadi kubwa ya watu huku Viongozi wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao Dk Willibrod Slaa pia aliyekuwa mbunge wa Arush Godbless Lema limekuwa na mada kali zinazotolewa katika mikutano hiyo ya hadhara.

Baadhi ya mambo yanayogusa vichwa vya mikutano hiyo ni pamoja na Ufisadi, Umasikini, utendaji wa chama tawala na utendaji mbovu wa viongozi wa nchi.

Akiogea katika mkutano wa hapo jana mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa hapo jana Alisema anashangaa kwa nini mawaziri wanaotoka katika mikoa hiyo wanakikumbatia chama tawala ilhali kimeshindwa kuwaletea wananchi mabadiliko, "Mimi ninawashangaa   wabunge wa majimbo ya Lindi na Mtwara wakiwamo (akiwataja kwa majina)   kwa nini wanakiunga mkono CCM wakati majimbo yao yamekithiri kwa umaskini,”

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi alisema wakati umefika kwa vijana kubadilika na kuhamia katika chama hicho huku akitoa mifano hai yenye kuonesha kinawajali watu wa hali ya chini ikiwemo uwezo wa yeye mtu wa hali ya chini kupata nafasi ya kugombea ubunge hali ambayo alisema huwezi kuikuta katika chama tawala.“Nawasihi vijana wenzagu kuungana na kuwa na ujasiri wa kuamua katika masuala ya kimaendeleo. Mimi nilikuwa mitaani na muziki wangu, lakini nikatokea Chadema na kunipa nafasi ya kugombea ubunge"

 Wakati huho huo Chama cha mapinduzi(CCM) ambacho ndiyo majeruhi mkubwa wa vuguvugu hilo leo kinatarajiwa kufanya mkutano wake wa hadhara katika eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taaarifa kutoka ndani ya Chama hicho kupitia kwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa huo, Juma Simba mkutano huo utahusu msimamo wa Chama hicho juu ya hatma ya maisha ya Watanzania, “Utaeleza hatma ya maisha ya Watanzania katika suala la ajira, miundombinu ya barabara, reli, bandari na anga, bei za bidhaa mbalimbali, umeme na rasilimali za taifa,” alisema Simba.

No comments:

Post a Comment