Monday, June 11, 2012

TAIFA STARS YAFANYA KWELI


Timu ya taifa 'Taifa Stars'imefanikia kuichapa Gambia kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hapoi jana na kuamsha nderemo kila kona ya nchi.
Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil taifa Stars walianza kutoka nyuma na kusawazisha kabla ya kufunga goli la ushindi. Gambi ndio walioanza kuongoza kupitia mchezajia wao Momodou Ceesay anayechezea klabu ya MSK Zilina ya Slovakia goli ambalo lilidumu mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza kilipomalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa Taifa Stars kushambulia huku Mabadiliko ya kumtoa John Boko na kumwingiza Haruna Moshi katika dakika ya 54 yaliongezakasi na nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Stars kwa nguvu na hatimaye katika dakika 60  beki Shomari Kapombe aliifungia Stars bao la kusawazisha akiunganisha kwa tik tak  krosi ya Erasto Nyoni.

Dakika zikiwa zinayoyoma mchezaji Erasto Nyoni aliyecheza kwa umahiri mkubwa hapo jana alifunga bao la pili lililoipa Stars ushindi kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 85, baada ya mchezaji wa gambia kunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Kwa matokeo hayo Tanzania sasa inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu na ikiwa pointi moja nyuma ya vinara Ivory Coast yenye pointi nne baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Morocco inayoshika nafasi ya tatu na Gambia inashika mkia ikiwa na pointi  mbili.

No comments:

Post a Comment