Saturday, January 11, 2014

CHELSEA YAIUA HULL CITY NYUMBANI NA KUJIKITA KILELENI!




London-Uingereza, Timu ya chelsea chini ya kocha Jose Mourinho imepanda kileleni mwa ligu kuu ya Baclays baada ya Leo hii kuifunga Hull City kwa mabao 2-0,wafungaji wakiwa ni Eden Hazards na Fernando Tores wote wakifunga katika kipindi cha pili.
Goli  la pili la Chelsea
 Mechi hiyo ilianza kupata msisimko katika dakika 23 pale kipa wa Chelsea Petr Cech alipofanya kazi ya ziada kuokoa mpira ambao almanusura uwapatie hull city bao la kuongoza.

Chelsea walipata bao lakuongoza katika dakika ya dakika ya 11 baada ya kipindi cha pili kupitia mchezaji wake Eden Hazard aliyemalizia pasi nzuri kutoka kwa Ashley Cole, ambapo alipiga shuti la chini chini katika kona na mpira kujaa nyavuni.
Goli la pili la Chelsea lilifungwa na Tores katika dakika ya 87 akionesha umahiri katika kugeuka na kupiga shuti la ambalo lilimshinda kipa wa Hull City.

Kwa matokeo  hayo Chelsea wamefikisha pointi 46 na kupanda mpaka nafasi ya kwanza huku ufalme wao katika nafasi hiyo ukitegemea matokeo ya Arsenal na Manchester city ambazo zipo nyuma kwa mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment