Wednesday, January 29, 2014

Lowassa ameanza safari ya Urais.

 
Ile ‘safari ya Lowassa’ imeibua mambo na mjadala mzito ndani na nje ya CCM.  Jambo la kujiuliza, je, safari hiyo ina urefu na vikwazo kiasi gani?
0Sha“Nimefarijika sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu…WanaCCM msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu zetu... Wingi wenu huu unanipa faraja katika safari yetu na kwa kumtegemea Mungu tutashinda.”  ni kauli ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa. 
\
Lowassa alitangaza hivi karibuni kuanza rasmi kwa safari hiyo aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo anasema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, majisafi na maendeleo ya uhakika.
Alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini mkoani Arusha.
Bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, Lowassa anawataka waliohudhuria ibada hiyo waungane na kaulimbiu yake, ‘Tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja’.
Hafla hiyo ya kimkakati, ilihudhuriwa  na baadhi ya wabunge, wengi wakiwa wa CCM, wenyeviti wa mikoa kadhaa wa chama hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM, viongozi wa jumuiya za chama na wengineo.
Licha ya kutoweka bayana aina ya safari anayoanza, Lowassa ni miongoni mwa wanaCCM wanaotajwa kuwa wanaowania urais, kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Dalili hizi za Lowassa kuutaka urais na kutafuta kabla ya kipenga kupulizwa, zimeishtua CCM na kumtahadharisha kuwa atapoteza sifa ya kupitishwa ifikapo 2015.
Safari tangu 1995
Tamaa ya Lowassa kuutaka urais haikuanza leo wala jana, ni ya tangu 1995 alipojitokeza kwa mara ya kwanza. Mwaka huo alikuwa miongoni mwa wagombea 17 wa CCM walioomba kuteuliwa kuipeperusha bendera ya chama hicho.
Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na vikao vitatu vya CCM –Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Kikao cha kwanza kilikua ni Kamati Kuu ambacho Mwenyekiti wake alikuwa Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Ali Hassan Mwinyi lakini Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa bado na ushawishi na nguvu kubwa ndani ya chama hicho.
Nyerere bila kumung’unya maneno, alisema wazi akiwataja wazi Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela kuwa hawakuwa wanafaa kugombea.
Nyerere alisema Malecela alikuwa na madhambi mengi na kwamba alikuwa ameyabainisha katika kitabu chake cha ‘Uongozi na hatima ya Tanzania’ ambacho pia alielezea udhaifu wa Horace Kolimba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.

No comments:

Post a Comment