Tuesday, May 29, 2012

MLIPUKO MKUBWA WATOKEA TENA KENYA!

NAIROBI,KENYA, Mlipuko mwingine umetokea sehemu yenye maduka mengi  katikati ya jiji la Nairobi karibu na Chuo kikuu cha Mount Kenya na kujeruhi watu wapatao 16 kwa mujibu wa  polisi.
habari zilizotolewa leo na chanzo cha polisi zimesema mlipuko huo umetokana na bomu.
Mlipuko mkubwa ulitokeamnamo saa 7:10 mchana saa za Afrika mashariki katika moja ya majengo yaliyopakana na maghorofa maeneo hayo , baadhi ya mashuhuda wamesema wanamhisi mtu aliyekuwa na begi aliyekuwa akija na kuondoka  eneo hilo.
Majeruhi walionekana wakipewa huduma na watu wa afya ambao walijaribu kuwaondoa mamia waliokusanyika katika eneo hilo kama mashuhuda.Picha za televisheni za Kenya zilionesha moshi mkubwa ukitoka katikakati ya majengo hayo.
Ingawa bado haijathibitka imeaminiwa kuwa kundi la kigaidi la nchini Somalia la Al-Shabab limehusika na mlipuko huo.Kundi hilo liliahidi na limehusika kutekeleza mashambulio kama hayo yaliyotokea nchii humo hivi karibuni, baada ya serikali ya Kenya kuingia nchini Somalia kwa lengo la kuendesha operesheni ya kulisambaratisha kundi la Al-Shabab.

VURUGU ZAENDELEA ZANZIBAR.

Vurugu zilizozuka tangu juzi na kutulia kwa muda zilizuka tena hapo jana baada ya  Mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki), Sheikh Musa Juma Issa kurudishwa rumande. Vijana waliokuwa wakipinga kurudishwa rumande kwa Mhadhiri huyo walichoma matairi barabarani na kuzua
 tafrani.
Vurugu hizo zimetokea baada ya utulivu uliojitikeza baada ya Dk Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuitisha mkutano uliojumuisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi wa vurugu hizo.
Hata hivyo kitendo cha kurudishwa rumande kwa Sheikh Issa aliyeshindwa kutimiza masharti ya dhamana kulizua vurugu tena  katika maeneo ya Mwanakeretwe na  Amani .

Polisi walilazimika kutuliza vurugu hizo kwa kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya vijana hao

Hadi jana jioni, maeneo ya Chumbuni, Amani, Mwembaladu hali ilikuwa bado tete huku polisi wakifunga barabara kwa ajili ya kudhibiti vijana hao.

Sunday, May 20, 2012

DROGBA AIPA CHELSEA UBINGWA KLABU BINGWA ULAYA!

Mmiliki wa Kalbu ya Chelsea Abahamovich akinyanyua kombe
Mashujaa wa jana Didier drogba na Kipa Peter Cech.

ALLIANZ ARENA, MUNICH,UJERUMANI, Hatimaye Chelsea wamefanikiwa kufuta machozi na maumivu waliyoyapata miaka minne iliyopita katika fainali za UEFA baada ya hapo leo kufanikiwa kutwaa kombe klabu bingwa Ulaya.

Alikuwa ni yule yule mkongwe aliyetegemewa Didier Drogba ndiye aliyeiongoza timu yake kutwaa ubingwa baada ya kufunga goli la kusawazisha na lile la ushindi katika Penati ya mwisho.

Buyern Munich ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la Chelsea katika dakika ya 83 kupitia kwa Thomas Muller, lakini dakika tano baaadaye katika dakika ya 88 Drogba akaisawazishia timu yake goli hilo kupitia mpira wa kichwa.
Thomas Muller akifunga goli.



Drogba akifunga goli la Kusawazisha kwa Chelsea.

Baada ya dakika 90 kuisha matokeo yalibaki kuwa 1-1 na hata baada ya Dakika 30 kuongezwa bado hali ilibaki hivyo na ndipo walipoingia katika mikwaju ya penati.


Katika Mikwaju hiyo Bayern ndiyo walikuwa wa kwanza kupiga ambapo ilikuwa kamifuatavyo:

 Philipp Lahm   alifunga, akafuata Juan Mata(Chelsea)-Akakosa, akafuata Mario Gomez(Bayern Munich)-akafunga, akfuata David Luiz(Chelsea)-akafunga, Manuel Neuer(Bayern)-akafunga,Frank Lampard(Chelsea) -akafunga, Ivica Olic(Bayern)-akakosa,Ashley Cole (Chelsea)-akafunga, Bastian Schweinsteiger (Bayern)-akafunga, na kisha Didier Drogba(Chelsea) -akafunga penati ya Ushindi.


Chelsea wakishangilia baada ya Penati ya mwisho.

Wachezaji wa Bayern wakigugumia kwa machungu.

Friday, May 18, 2012

MKUTANO WA G8 WAANZA:

 MAREKANI, Mkutano wa nchi tajiri za kwa viwanda umeanza hapo jana huko Camp David,Maryland, Marekani ambapo moja ya Ajenda muhimu ni usalama wa chakula Afrika na hali ya uchumi ulaya hasa katika nchi zenye migogoro ya kiuchumi ikiwemo Uturuki na Ugiriki.
Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha viongozi wa Uingereza,Ufaransa,Ujerumani,Italia,Japan,na Marekani ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo.

Moja ya ajenda katika mkutano ni pamoja na Hali ya uchumi Ulaya, Hali ya nyuklia Iran, Hali ya Syria, Pia usalama wa chakula na nishati duniani ikiwemo Afrika.

Hata hivyo licha ya ajenda hizo bado wengi hawana matumaini na mkutano huo kwani iliyotangulia haikuzaa matunda kama ilivyotegemewa.

MAELFU WAKIMBIA MAPIGANO DRC

Moja ya kundi la wakimbizi wakiwa njiani Goma.

Bunagana, DR Congo - Mapigano yanayoendelea huku Kivu Kaskazini mashariki ya Kongo yamewalazimisha wakazi wa maeneo hayo kukimbilia nchi za jirani za Rwanda na Uganda kuokoa maisha yao.Wanawake na watoto ni moja ya kundi kubwa katika msafara huo.


Wananchi hao wanakimbia kuhofia kushambuliwa na waasi wanaoipinga  serikali ya kinshasa wakiongozwa naaliyekuwa kamanda wa jeshi la kongo Jenerali Ntaganda.
Tumesikia mapigano kati ya waasi na Serikali, kwa hiyo tumekimbia huku kujiokoa kwa sababu kubaki kule ni kuhatarisha maisha yetu" alisema kajambere seberera  ambaye yupo nchini Uganda baada ya kukimbia mapigano hayo.


Hata  hivyo hali sio nzuri katika kambi za UNHCR  Kisoro nchini Uganda ambapo licha ya kufunguliwa sehemu hiyo bado chakula, malazi na maji vimekuwa ni tatizo.Baadhi ya wakimbizi hao wamelazimika kulala nje huku wengine wakirudi Kongo mchana kutafuta maji na Chakula.


Hali imekuwa ngumu zaidi kwa watoto na akinamama waliovuka mipaka ambao idadi yao ni kubwa.


Mapigano hayo kati ya majeshi ya serikali na yale ya majeshi ya Kamanda muasi Jenerali Ntaganda yalianzayamesababisha usumbufu mkubwa katika eneo hilo la Kivu na maeneo menginene nchini humo.

MKURUGENZI WA TBS ASIMAMISHWA KAZI.

Mkurugenzi wa TBS Charles Ekerege.
 Dar es Salaam, Siku chache baada ya kuteuliwa waziri wa viwanda Mh.Abdallah Kigoda ametoa maagizo ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi mkuu wa shirika la Viwango tanzania TBS Bw Charles Ekelege. Akiongea na waandishi wa habari hapo juzi Waziri kigoda amesema Moja ya sababu za rais kuamua kuvunja baraza la mawaziri lililokuwepo ni pamoja na tuhuma nzito zilizokuwa zikielekezwa TBS hivyo ni vyema mkurugenzi huyo akasimamishwa kupisha uchunguzi na hatua zaidi za kisheria.


Wachunguzi wa mambo wanahisi hiyo ni sehemu ya ahadi alizotoa rais Kikwete katika hotuba yake siku alipokuwa akitangaza baraza jipya la Mawaziri ambapo aliahidi kuwawajibisha watendaji wa ngazi za chini pia ambao mara nyingi ni chanzo cha mawaziri kuwajibika.

Imekuwa ni kawaida kwa watendaji wengi wa ngazi za chini katika wizara kuzembea kwa kuelewa kuwa wao sio wawajibikaji wa moja kwa moja zitokeapo tuhuma pengine hatua hizi zitasaidia.

MPENDWA PATRICK MAFISANGO AAGWA TCC.

Mwili wa mafisango Ukiwa Umebabwa na wachezaji wenzake.
Juma Kaseja Akilia Kwa uchungu.
Mdogo wa marehemu Akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu.
Kocha wa Simba Milovan.
Dar Es Salaam, Mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Simba na timu ya taifa ya Kongo, Patrick Mutesa Mafisango umeagwa rasmi katika viwanja vya TCC Chng'ombe Jijini dar es Salaam,na mamia ya wanamichezo wakiongozwa na waziri wa michezo Dr.Fennela Mukangala.

Waombolezaji wengine(Picha zote kwa hisani ya millardayo.com na Global Publishers)
Wengi wa mashabiki na wapenzi hao wa soka walionekana kuwa na majonzi huku wachezaji wenzake,pamoja na kocha wa Timu ya Simba Milovan wakishindwa kujizuia kwa machozi.

mwili wa mafisango umesafirishwa jioni ya Ijumaa hii kuelekea nyumbani kwao Nchini Kongo kwa ajili ya mazishi yatakayofanyka siku ya Jumapili mchana.

Patrick mafisango mchezaji wa timu ya Simba na Timu ya taifa ya Kongo alikuwa mfungaji namba tatu wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu na alikuwa na msaada mkubwa katika kufanikisha Timu ya Simba kupata ubingwa Msimu huu, Anga za Kimataifa Inaungana na wadau wote wa Michezo pamoja na familia ya marehemu Kumuombea heri ; MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, AMEN.

SINGLE BOY OFFICIAL VIDEO-ALI KIBA FT JAY DEE.

Tuesday, May 15, 2012

MAGAIDI WASHAMBULIA HOTELI KENYA.

Polisi akilinda eneo la tukio usiku huu.

Magaidi wameshambulia hoteli maarufu ya Bella Vista Restaurant,iliyopo pembezoni mwa bara bara ya kwenda Mombasa na kuua mtu mmoja huku wakijeruhi wengine watano.
Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na milipuko mitatu katika klabu hiyo ya Bella Vista Restaurant ambayo ni kutoka katika guruneti zilizorushwa kuelekea hotelini hapo.
Milipuko hiyo ilisababisha uharibifu wa magari sita yaliokuwa yameegeshwa kando ya hoteli hiyo.
Mkuu huyo wa polisi alisema wanaamini shambulio hilo lilitekelezwa na magaidi.

Inadaiwa kuwa watu wawili walikwenda katika Klabu hicho wakitaka kuruhusiwa kuingia.
Lakini walipotakiwa kukaguliwa  na maaskari wa hoteli hiyo walikataa na ndipo wakarusha maguruneti hayo.
 Mmoja wa watu waliokuwa karibu na eneo hilo ameiambia AFP kuwa aliwaona watu wakikimbia baada ya mlipuko mkubwa.
mashuhuda wa tukio wamedai watu hao walifyatua risasi hovyo wakati wakiondoka huku polisi wakisema bado hawajamkamata mtu yeyote kuhusianan na tukio hilo.

Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya milipuko ambayo yamelenge vituo vya polisi, |Makanisa na baa za pombe hivi karibuni baada ya kenya kuivamia Somalia na kupambana na wanamgambo wa Alshabab, na pengine tukio hili litahusishwa na kikundi hicho


Monday, May 14, 2012

RAIA WA SUDAN KUSINI WARUDI NYUMBANI

JUBA SUDAN KUSINI- Hatimaye ndege ya kwanza iliyowabeba wakimbizi waliokwama kwa miezi kadhaa nchini Sudan imewasili mjini Juba Sudan Kusini. Raia hao wapatao 164 wanatarajia kusafirishwa kwa barabara hadi katika kambi mpya wakisubiri kutafutiwa jamaa zao.
Kundi hili ni la raia laki tano ambao walipoteza uraia wao baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake mwaka jana. Nchi hizo nusura kuingia vitani kutokana na mzozo wa raslimali za mafuta na mipaka.
Raia waliofika leo wamekuwa katika jimbo la Nile ambapo walipewa hadi Mei 20 kuamua ikiwa watachukua uraia wa Sudan au kurejea Sudan Kusini.
Maafisa wa Sudan wamepinga hatua ya kuwasafirisha raia hao kwa wingi kwa hofu ya usalama.
Punde baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake maelfu ya raia wake waliofanya kazi katika iliyokuwa serikali ya taifa moja la Sudan waliachishwa kazi na utawala wa Khartoum.
Kuna kambi maalum mjini Juba ya raia hao kabla ya kutafuta maeneo yao ya asilia.
Maelfu ya raia wa Sudan Kusini walihamia Kaskazini wakati wa vita na kutafuta ajira.

Sunday, May 13, 2012

NI MANCHESTER CITY!!


Manchester-UINGEREZA,
Magoli mawili ya dakika za nyongeza yameileta miujiza isiyokuwa ikitegemewa na wengi na kuifanya timu ya Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka 1968. Magoli ya  Edin Dzeko na Sergio Aguero dhidi ya QPR katika dakika za nyongeza yalifufua matumaini ya Manchester City ambayo mpaka dakika 90 ilikuwa nyuma kwa goli moja. Mpaka mapumziko Manchester city walikuwa wakiongoza kwa goli moja la Zabaleta, lakini mambo yalibadilika katika kipindi cha pili baada ya Mchezaji wa QPR Cisse kusawazisha kabla ya Mackie kuongeza goli la pili kwa QPR akimalizia kwa kichwa krosi safi kutoka kwa Traore.

Manchester City wamekuwa mabingwa wapya baada ya kufikisha pointi 89 sawa na mahasimu wao wakubwa Manchester United lakini wao wapo mbele kwa magoli.

Bidii binafsi za wachezaji Yaya Toure na Balotel zilioonekana dhahiri kuzaa matunda kwa timu hiyo.

Huko ujerumani nako timu ya Borushia Dotmund ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya nchi hiyo.

HAPPY MOTHER'S DAY!!

Heri ya siku ya mama, Anga za kimataifa inaungana na wote wenye mapenzi mema na wenye kuutambua na kumheshimu mama kama mlezi wa msingi, mwenye mapenzi ya dhati na mlinzi dhabiti wa familia na jamii kwa ujumla.

Monday, May 7, 2012

Hollande Ambwaga Sarkozy Kinyang'anyiro cha urais Ufaransa

Rais aliyekuwa madarakani nchini Ufaransa Bw.Nicolas Sarkozy ameshindwa kutetea kiti chake hichobaada ya kushondwa katika uchaguzi mkuu nchini humo na hivyo kushindwa kuendelea na muhura wa pili wa nafasi yake hiyo. 
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na vyombo vya habari baada ya zaidi ya asilimia 95 ya kura zote kuhesabiwa  yanaonesha Bw Hollande amejipatia asilimia 51.9 za kura akimshinda mpinzani wake Bw. Sarkozy aliyepata asili mia 48.1.


Shamra shamra nyingi zimeendelea nchini Ufaransa huku wachambuzi wa mambo wakisema wananchi wengi walitaka rais huyo aondoke kutokana na kuwa na sera mbovu za ndani na nje.
Hata hivyo rais huyo Sarkozy amewashukuru wafuasi wake na kukubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzihuo,  huku akiweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza kuondolewa madarakani baada ya muhura mmoja.

Rais Mteule Bw. Francois Hollande anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo na kukabidhiwa ofisi rasmi kutoka kwa Bw.Sarkozy.

Thursday, May 3, 2012

UJUMBE WA BAN KI- MOON KUADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI:


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki-moon akiwa  na Mkurugenzi  Mkuu wa UNESCO Bi Irina Bokova kwa katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani .

 

 

Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kasi na yenye nguvu, uhuru na uongezekaji kwa wingi wa vyombo vya habari sio suala linalozuilika.

 

 Mwaka uliopita mapinduzi huko Afrika kaskazini na mashariki ya kati, pia katika mitandao ya kijamii,simu na satelaiti yamefanya kazi kubwa kutengeneza mlolongo wa mabadiliko kutoka kwa muuza mboga za majani masikini aliyekuwa analilia utu wa kibinadamu mpaka kuanguka kwa tawala za kidiktekta na kuleta uwezekano wa mamilioni ya watu kwa mara ya kwanza kufurahia demokrasi na nafasi walizokuwa wakinyimwa.

 

 Hiyo ndiyo inayoelezewa kama dhima iliyobeba ujumbe wa uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu; Sauti mpya: Uhuru wa vyombo unasaidia kubadilisha jamii.

 

Chombo huru cha habari kinawapa watu taarifa wanazozitaka ili kufanya maamuzi muhimu kuhusu maisha yao. Pia kinawawajibisha viongozi na kuweka wazi rushwa, kuongeza uwazi katika maamuzi. Pia chombo huru cha habari kinafungua ufahamu na kutoa matokeo ya sauti mbalimbali hasa zile ambazo pengine zisingesikika.

 

Lakini uhuru wa vyombo vya habari bado umebakia wenye uchungu.kila siku waandishi wa habari  wanapo fanya kazi zao wanakutana na vitisho vyenye kuogofyaa. Mwaka uliopita zaidi ya waandishi 60 waliuawa duniani kote, na wengine wengi kujeruhiwa.Kama kwa mujibu wa kamisheni ya kuwalinda waandishi wa habari mpaka Desemba, 1 mwaka jana kuna waandishi 179 wa habari walikuwa wakizuiliwa.Hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 20 zaidi ya mwaka 2010, na kubwa zaidi tangu 1990.

Idadi nyingine kubwa ya waandishi wa habari walifungiwa na kunyamazishwa na serikali, mashirika na watu wenye nguvu.huku uhuru kwa wale wanaowashambulia waandishi wa habari ukionekana wazi.


 Nina wasiwasi kuwa mashambulizi dhidi  ya waandishi wa habari yapo yanakua kwa sasa. Natoa wito kwa wahusika wote kuzuia na kuzichukulia hatua za kisheria vurugu hizi. Watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari wanatetea haki zetu sisi ni lazima tulinde zao pia.


Mwezi wa eptemba mwaka jana umoja wa mataifa uliitisha kwa mara ya kwanza mkutano wa wadau kuhusu usalama wa waandishi wa habari.mkutano ulizaa mpango kazi dhabiti, na mfumo wa umoja wa mataifa kwa sasa unakusanya na kuimarisha nguvu zetu kuongeza ufahamu juu ya mambo haya, unasaidia  wanachama kuimarisha mifumo ya kisheria na kuwashawishi kuchunguza visa vya mashambulio dhidi ya waandishi.

 

 Tunapoadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari, tuhaidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha waandishi wanafanya kazi zao katika mazingira mapya na ya yenye kuendana  na uandishi ..... ambayo yataleta mchango muhimu katika jamii Imara,yenye afya na yenye amani zaidi