Monday, May 7, 2012

Hollande Ambwaga Sarkozy Kinyang'anyiro cha urais Ufaransa

Rais aliyekuwa madarakani nchini Ufaransa Bw.Nicolas Sarkozy ameshindwa kutetea kiti chake hichobaada ya kushondwa katika uchaguzi mkuu nchini humo na hivyo kushindwa kuendelea na muhura wa pili wa nafasi yake hiyo. 
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na vyombo vya habari baada ya zaidi ya asilimia 95 ya kura zote kuhesabiwa  yanaonesha Bw Hollande amejipatia asilimia 51.9 za kura akimshinda mpinzani wake Bw. Sarkozy aliyepata asili mia 48.1.


Shamra shamra nyingi zimeendelea nchini Ufaransa huku wachambuzi wa mambo wakisema wananchi wengi walitaka rais huyo aondoke kutokana na kuwa na sera mbovu za ndani na nje.
Hata hivyo rais huyo Sarkozy amewashukuru wafuasi wake na kukubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzihuo,  huku akiweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza kuondolewa madarakani baada ya muhura mmoja.

Rais Mteule Bw. Francois Hollande anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo na kukabidhiwa ofisi rasmi kutoka kwa Bw.Sarkozy.

No comments:

Post a Comment