Wednesday, April 4, 2012

CHADEMA WAIBUKA KIDEDEA ARUSHA

Arumeru,-Arusha,

 Hatimaye matokeo ya uchaguzi wa Ubunge kupitia jimbo la Aremeru Mashariki yametangazwa na mgombea kupita cham cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joshua Nassari kuibuka kidedea na kumbwaga mpinzani wake mkuu bw. Sioi Sumari kwa tofauti ya kura 6215.Nassari amepata asilimia 54.91 ya kura zote wakati mpinzani wake wa karibu, Sioi Sumari wa CCM alipata asilimia 44.56 ya kura halali 60,038 zilizopigwa katika vituo 327 vya kupigia kura..


Akimtangaza mshindi huyo msimamizi wa uchaguzi wa mkurugenzi wa wilaya ya Arumeru bw.Gracias agenzi amemtangaza Sioi kuwa mshindi baada ya kupata jumla ya kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Bw.Sioi Sumaria aliyeambulia jumla ya kura 26,757.

Pia alitangaza matokeo kwa vyyama vingine vilivyoshiriki ambapo chama ch DP kilipata kura 77, NRA kura 35 AFP kura139,UPDB kura 18,TP kura1 8 na SAU kura 22.

 Bw. Kagenzi  alieleza kuwa zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliyejitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 karibu  nusu ya waliojiandikisha, ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni 661.

Wakati huo huo  CHADEMA imeendelea kufanya vizuri katika uchaguzi wa madiwani ambapo kimefanikiwa kupata ushindi katika kata za kirumba -Mwanza, pia Songea na Mbeya




No comments:

Post a Comment