Sunday, April 1, 2012

Taarifa Kwa Wahitimu Wote wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mwaka 2011
Monday, 26 March 2012 05:24

Wahitimu wote wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa mwaka 2011 wanaarifiwa kuwa vyeti vyao vya kitaaluma (Academic Transcripts) na vile vya kuhitimu masomo (Certificates) vipo katika hatua za mwisho za kuhakikiwa na kuchapishwa. Kutokana na ubora wa vyeti hivyo, zoezi hilo sio la muda mfupi. Vyeti vinatarajiwa kuwa tayari katikati ya mwezi Aprili 2012.

Pia, wahitimu wote waliorejesha majoho na hawakurudishiwa fedha zao, kwamba fedha hizo sasa zitarejeshwa kupitia akaunti zao za benki kuanzia tarehe 31 Machi 2012.

 ...Kwa taarifa zaidi Tembelea website ya chuo www.udom.co.tz 

No comments:

Post a Comment