Monday, April 23, 2012

WAANGALIZI WA UMOJA WA MATAIFA WAONDOKA IRAN


VIENNA/TEHRAN |
Waangalizi wa umoja wa mataifa waameondoka leo nchini Iran baada ya kukataliwa na Iran kukagua maeneo muhimu ya siri yanayohisiwa kutengeneza silaha za Nyuklia hali ambayo inaweza kuongeza mvutano kati yake na mataifa ya Magharibi.
Marekani imeishutumu Iran na kusema kwa mara nyingine tena nchi hiyo imeka
taa kutimiza wajibu wake wa kimataifa katika mpango wake huo wa nyuklia.


Iran kwa upande wake kupitia kwa kiongozi mkuu wa kidini Bw.Ayatollah Ali Khamenei Imesema sera za iran kuhusu mpango wake wa nyuklia hazitabadilika licha ya mkandamizo kutoka kwa nchi za magharibi zinazoutuhumu mpango huo kama wa kutengeneza silaha
za maangamizi, "Kwa msaada wa Mungu na bila kujali propaganda, mpango wa nyuklia wa iran utaendelea kwa uimara na Umakini" alisema kiongozi huyo akiongeza kuwa vikwanzo na mauaji hayatazaa matunda katika kuukwamisha mpango huo.


Timu ya wataalamu kutoka Vienna ya kuchunguza Nguvu za atomiki IAEA ilikuwa nchini Iran ikitegemea kukagua sehemu ya Parchin ambapo ndipo kunaaminika kuwepo kwa vifaa vya majaribio ya milipuko lakini IAEA imesema Iran imewazuia kufika sehemu hiyo.
Kukataliwa huko timu hiyo kunaweza kuongeza msuguano zaidi na hati hati ya kuvunjika kwa kwa mapatano ya mradi huo wa nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yakiwemo Marekani,China, Uingereza, Urusi,Ufaransa na Ujerumani.

No comments:

Post a Comment