Sunday, April 1, 2012

HATIMAE LOWASA AMNADISIOI

Arumeru,
hatimaye waziri mkuu mstaafu Mh.Edward Lowassa amejitokeza na kumnadi mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni ndani ya kijiji cha Katiti huko Arumeru.

Katika mkutano huo Lowassa aliwataka wananchi kukipigia kura chama cha CCM akiwaahidi kuwa kero za maji, ardhi na Umeme zitakwisha muda watakapomchagua mgombea huyo.

“Nimekuja hapa kuwatangazia ikiwa mtakichagua CCM  mjadala wa kero  zinazowakabili utafungwa katika uchaguzi huu mdogo,” alinukuliwa Lowassa.

Huku akiongeza;
“Ni juzi tu Rais alitoa mamia ya ekari kwa wenzenu hawezi kushindwa kuwapa hata nyie ipeni kura CCM na mtaona,“ alisema akimaanisha ekari 5000 zilizotolewa na rais kikwete kwa wananchi wa Arumeru magharibi.

Lowassa pia alisisitiza wananchi kuichagua CCM kwa kuwa inalinda misingi ya amani huku  akivituhumu vyama vya upinzani kwa kuchochea vurugu.

Hii inakuwa ni mara ya Kwanza kwa Waziri mkuu huyo mstaafu kupanda jukwaani baada ya kudaiwa kuwepo kwa mivutano ya chini kwa chini na uwezekano wake wa kutojitokeza katika kampeni hizo.

katika kampeni hizo pia Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.benjamin William Mkapa alipanda jukwaani huko Patandi - Tengeru   ambapo katika hotuba yake alielezea kusikitishwa na vijana wanaoibeza CCM akisisitiz CCM imefanya mengi katika miaka 50 ya Uhuru.

“Ninasikitishwa sana na vijana wetu wa leo kukukubaliana na wendawazimu wanaosema kuwa Serikali haijafanya lolote katika taifa hili, tumejenga shule za msingi na sekondari na ndiko mlikosoma na leo kweli mnaweza kukubaliana na Chadema?," aliuliza Mkapa.

“Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanya kazi kubwa sio kwa taifa hili peke yake lakini hata kwa kusadia ukombozi wa mataifa mengine barani Afrika,” 

Kampeni za Ubunge zilikuwa zikifikia kikomo kusubiri uchaguzi hapo Tarehe 1 Aprili siku ya Jumapili.

  

No comments:

Post a Comment