Monday, April 16, 2012

WAASI WACHUKUA MJI MUHIMU WA MAFUTA LIBYA.

Wakipigana na majesh ya Mouammar Ghadaffi waasi nchin Libya wamefanikiwa kuuteka mji muhimu waenye Mafuta wa Begra uliopo pwani ya Bahari ya mediteranian. Msemaji wa jeshi la waasi Al-Rijal amesema wamefanikiwa kuchukua Mji huo uliopo kilometa 200 kutoka ngome kuu ya waasi  ya Benghazi baada ya mapigano ya wiki tatu mfululizo, 'Begra imekombolewa' alisema Al-Rijal.
Taarifa kutoka katika mji wa Brega zinasema kuwa katika mapambano ya usiku wa kuamkia juzi, zaidi ya wapiganaj waasi saba wamepoteza maisha huku wengi 44 wakijeruhiwa na kuongeza kuwa wanajeshi 20 wa Kanali Gaddafi wamejisalimisha kwa vikosi vya waasi.
Licha ya kushikilia baadhi ya maeneo katika mji huo waasi hao wameendelea pia kupata upinzani katika mji Misrata, mji ambao wameongeza mashambulizi kutaka kuuweka chini ya himaya yao kiti ambacho kimeonekana kutowezekana kwa sasa.
Mashambulizi ya waasi yaliongezewa nguvu na vikosi vya majeshi ya NATO miezi mitano iliyopita ambapo yamekuwa mashambulizi ya anga kwenye kambi za wanajeshi wa Seriali huku wachambuzi wa mambo wakisemakuwa vikosi hivyo vimeshindwa kumuangusha Kanali Muammar Gaddafi.
Siku ya Alhamisi mamia ya waasi waliuteka Mji mdogo wa Nasser kilometa 25 kutoka mji wa Zawiya baada ya masaa kadhaa ya mapigano, Zawiya ni mji  wa karibu kabisa kuelekea Ngome kuu ya Muammar Gadhafi ya Tripoli abao pia ni mji mkuu wa nchi hiyo.
Maduka yalifungwa katika mji wa nasser na inadaiwa na mashuuda kuwa waasi walivami kituo kimoja cha mafuta na kajuza magari na vifaru vyao kwa mafuta hayo.(

No comments:

Post a Comment