Tuesday, March 5, 2013

UCHAGUZI KENYA-MATOKEO YAENDELEA KUTOLEWA-KENYATTA BADO KINARA.

Baada ya siku kashikashi ya uchaguzi na kupiga kura  nchini Kenya, Matokeo ya uchaguzi huo yameazwa kutangazwa toka hapo jana. 

Matokeo hayo mpaka sasa yanaonesha Uhuru Kenyatta anaongoza kwa asilimia hamsini na tano(55%) huku mpinzani wake Raila Odinga akiwa na asilimia arobaini na moja(41%) , Musalia Mudavadi wa Peace Coalition asilimia 3 na vyama vingine vikipata asilimia 1 na vingine chini ya asilimia 1.

Wananchi wa Kenya Wakifuatilia matokeo hayo katika Televisheni.






       Ufuatao ni Muhtasari wa matokeo hayo:
  • Uhuru Kenyatta (Jubilee Alliance): 55%
  • Raila Odinga (Coalition for Reform and Democracy): 41%
  • Musalia Mudavadi (Peace coalition): 3%
  • Asilimia 37% ya vituo vya kupigia kura vimeshatoa matokeo.

No comments:

Post a Comment