Monday, March 4, 2013

UCHAGUZI KENYA WAFANYIKA LEO-WENGI WAJITOKEZA

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/66180000/jpg/_66180790_66180689.jpg 

NAIROBI-KENYA,
Wananchi wa Kenya wapatao milioni kumi na nne ambao wamejisajili kama wapigakura wameanza kutumia haki yao hiyo asubuhi hii huku wengi wakijitokeza mapema nayo Tume Huru ya Uchaguzi na Ukaguzi wa Mipaka IEBC ikiwanyooshea kidole wanaotaka kuvuruga uchaguzi.

Hii ni siku ya kihistoria kwa wananchi wa Kenya ambao wanapata nafasi ya kupiga kura kumchagua Rais wa Nne wa Jamhuri hiyo huku pia kwa mara ya kwanza wakichagua magavana na maseneta ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa katiba mpya.
Jeshi la Polisi nalo kupitia kwa msemaji wake Charles Owino limejigamba kuwa kamili kukabiliana na vitisho vya aina yoyote pamoja na ghasia ambazo zinapangwa wakati wa uchaguzi na hata pindi matokeo yatakapotangazwa.
msemajiwa jeshi hilo wake
Aidha Mwenyekiti wa IEBC Isaack Hassan akiongea na wanahabari kwa mara mwisho kabla ya kinyang'anyiro hicho katika kituo cha Bomas amewashukia wanasiasa ambao wameanza kulalama eti kina mpango wa kuwaibia kura.
Vituo vya kupigia kura nchini humo vimefunguliwa rasmi saa kumi na mbili asubuhi na vinatarajiwa kufungwa saa kumi na moja kamili jioni ndipo zoezi la kuhesabu kura lianze na matokeo kubandikwa kwenye vituo husika.

No comments:

Post a Comment