Tuesday, March 5, 2013

UCHAGUZI KENYA-POLISI AMPIGA RISASI MSIMAMIZI WA KITUO CHA KURA

Murang'a-KENYA,
 Katika hali isiyo ya kawaida polisi mmoja amemuua msimamizi wa kituo cha kupigia kura Bw.Waithanje Mwaniki katika jimbo la Kangema walipokuwa njiani wakirudi kutoka katika kituo cha kupigia kura na masanduku ya kura. 

Taarifa ya awali iliyotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo imesema polisi huyo alikuwa ndani ya gari na marehemu akiwa amekaa kiti cha nyuma ya Marehemu na alimpiga risasi hiyo kwa bahati mbaya.

Polisi huyo amekamatwa na uchunguzi ukiendelea ambapo utata zaidi umeligubika tukio hilo kutokana na msimamizi msaidizi wa kituo hicho kupotea baada ya tukio hilo na haifahamiki yupo wapi mpaka sasa<t>

No comments:

Post a Comment