Wednesday, February 29, 2012
KINYANG'ANYIRO MGOMBEA URAIS KUPITIA REPUBLICAN-MICHIGAN WAPIGA KURA.
Mitt Romney mgombea anayeongoza katika kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa kukiwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi ujao anasubiri hatima yake kutoka katika Jimbo la Michigan sehemu ambalo alipozaliwa kujua kama atanyanyuka kidedea au atatupwa katika mbio hizo. Romney anapata upinzani mkali kutoka kwa Rick Santom ambaye anakabana nae koo kabla ya upigaji kura hapo jana Jumanne.
Baada ya kushinda katika jimbo la Arizona ambako alipata msaada mkubwa kutoka kwa Seneta wa jimbo hilo na mgombea wa urais kupitia tiketi ya Republican mwaka 2008 Bw. John McCain, Romney anaiangalia Michigan kama moja ya mategemeo yake makubwa katika ushindi wake, huku maoni yakionesha mchuano mkali kati yake na mpinzani wake huyo wa karibu.
Endapo Santom atapata ushindi katika jimbo hilo litakuwa ni pigo kubwa mno kwa Romney na pengine itazua maswali mengi juu ya Uwezekano wa Romney kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo Romney anapewa nafasi zaidi dhidi ya Santom ambaye msimamo wake wa kidini na kutoaminika kama mgombea imara Dhidi ya Rais Obama vinampunguzia umaarufu.
Romney anaaminika kama Mchumi Imara kutokana na kuwa mfanyabishara maarufu akiwa na uzoefu wa miaka 25, na pia kushika nafasi ya Gavana.
Akiongea katika kampeni zake Romney alinukuliwa akisema "Nitakwenda kushinda Michigan na nitashinda Nchi nzima"
kwa Upande wake Santom alisema amevutiwa na ushindani uliopo tangu mwanzo wa safari na jana wangeushangaza ulimwengu. Wagombea wengine Bw.Newt Gingrich na Ron Paul wameonekana kuachwa mbali katika mbio hizo kwa kutoa upinzani hafifu ambao umewaondoa katika mjadala kama wagombea wenye mvuto na upinzani.
Mbio hizo ni za kumtafuta Mgombea Urais atakayepambana na rais aliyepo madarakani Bw.Barack Obama wa chama cha Democratic hapo Novemba Mwaka huu.
Sunday, February 12, 2012
WHITNEY HOUSTON AFARIKI!!
Whitney Elizabeth Houston - aliyezaliwa mwezi August 9, 1963 amekutwa akiwa amefariki katika Hoteli ya Beverly Hillton na kwa mujibu wa polisi wa Beverly Hills wamesema Whitney hakuna dalili za kuwepo kwa tukio la kihalifu lililosababisha kifo hicho ingawa pia chanzo cha kifo hicho hakijafahamika.
Whitney ambaye hivi karibuni alianza kurudi jukwaani tangu mwaka 2006 alipotalakiana na mumewe Bobby Brown baada ya ndoa yao ya miaka 14, wakiwa na mtoto wao Bobbi Kristina ,ambapo alifanikiwa kufanya wimbo mmoja na mwanamuziki Akon uliotambulika kwa jina la "Like I never Left" na katika siku za hivi karibuni kabisa akipata mwaliko wa kutumbuiza katika tamasha la utangulizi la utoaji wa uzo za Grammy kwa mwaka 2012 ingawa katika mazoezi sauti yake ilionekana kuwa dhaifu na isiyo na makali ya miaka ile tena.
Katika mafanikio yake whitney alivuma kama mwanamuziki bora wa kike duniani huku album zake zikishika chati za juu na kumuwezesha kuwa moja ya wasanii waliowahi kuuza zaidi duniani. Pia Whitney amewahi kuvuma katika anga za filamu ambapo alicheza katika filamu za "The Bodyguard" na "Waiting to Exhale" huku nyimbo zake zikitumika kama soundtracks na kumpatia mauzo ya kiwango cha juu.
Akiwa Binti mdogo Whitney mtoto wa muimbaji wa nyimbo za dini Cissy Houston na marehemu John Houston aligunduliwa kipaji chake na clive Davis aliyekuwa Producer katika lebo ya Arista Records mwanzoni mwa miaka ya 1980 ambaye alimuongoza kuuza jumla ya nakala milioni 170 za sauti na video huku nyimbo zake za "I will always love you" na " The Greatest Love of All".
Hata hivyo maisha ya mwanamuziki huyo baadae yalitawaliwa na matumizi ya pombe na dawa za kulevya hali iliyomuathiri afya yake.
Pamoja na yote Whitney Houston atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki ambao umewaathiri vizazi vya sasa wakiwemo wanamuziki Brandy, Monica, Mariah Carey, Beyonce na Christina Aguilera ambao wameiga mfano wake, pia atakumbukwa kwa kujishighulisha na masuala ya kijamii ikwemo haki za wamarekani weusi hasa katika masuala ya Elimu.
MwenyeziMungu mwenye Rehema ailaze mahali Pema Peponi roho ya mpendwa wetu Whitney Houston Amen!
LA LIGA:BARCELONA WABANWA NA OSASUNA
Hispania,
dejan lekic hapo jana aliisaidia timu yake ya Osasuna kuiangusha moja ya miamba ya soka Nchini Hispania Barcelona kwa jumla ya magoli 3-2.
Osasuna walipata goli lao la kwanza kupitia kwa mchezaji huyo Dejan katika dakika ya sita ya kipindi cha kwanza.Dakika 16 baadae katika dakika ya 22 Osasuna waliongeza goli lao la pili kupitia kwa mchezaji yule yule Dejan na kuwafanya waende mapumziko wakiongoza kwa magoli 2-0.
Baada ya mapumziko kocha wa Barcelona alifanya mabailiko na kumuingiza Kapteni Carles Puyol abaye aliongeza nguvu na kuwafanya Barcelona kupata goli katika dakika ya 6 ya kipindi cha pili kupitia kwa Alexis ssanchez ingawa furaha hiyo haikudumu kwani dakika ya 73 mchezaji Raul Garcia aliiandikia timu yake goli la tatu.
Zikiwa zimebaki dakika chini ya 20 mchezo kumalizika barcelona waliongeza bidii na kufanikiwa kupata goli la pili baada ya Cesc Fabregas kumtumbukizia Mpira Christian Tello ambaye hakufanya ajizi na kufunga goli hilo.
Baada ya goli hilo matokeo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo na kuwafanya Barcelona wakizidi kuachwa katika msimamo wa ligi hiyo na Mahasimu wa Real Madrid kwa Point saba huku Madrid bado wakiwa na mchezo mkononi.
CHELSEA HOI KWA EVERTON- yafungwa 2-0, Pienaar awa mwiba.
Mchezaji wa afrika Kusini Steven Pienaar alikuwa mwiba mkali Everton ilipoichapa Chelsea Kwa magoli 2-0, akifunga goli la kwanza huku lile a pili likifungwa na Muagentina denis Stracqualursi katika kipindi cha pili.
Evertonambao hapo jana walikuwa wenyeji katika uwanja wao wa Goodison Park walianza kwa kasi na kufanikiwa kuapata goli lao la kwanza katika dakika ya 5 baada ya mpira uliomgonga Frank lampard Kumkuta Pienaar ambaye alipiga shuti kali la karibu lililomshinda kipa Petr Cech.
Everton nusura wapate goli la pili katika dakika ya 18 wakati Petr Cech aliposhindwa kuondoa mpira katika hatari na kumkuta Landon Donovan nje kidogo ya kumi na nane amabapo hata hivyo shuti lake hafifu liliokolewa na kipa huyo.
Chelsea nao walijitahidi kuongeza nguvu katikati mwa kipindi cha kwanza ambapo walikaribia kupata goli katika nafasi mbili ya kwanza katika dakika ya 25 ambapo shuti la michael Essien liliokolewa na Mlinzi wa Everton na lile lililofuatia la daniel Sturridge liliokolewa pia, huku nafasi nyingine ya Juan Mata ambaye alipiga shuti baada ya kupokea mpira kutoka kwa Sturridge ndani ya Eneo la penati liliishia kumgonga mlinzi wa Everton na kuwa Kona.
Hata hivyo chelsea walishindwa kuendeleza mikiki mikiki hiyo katika kipindi cha pili na kujikuta wakifungwa goli la pili dakika ya 72 katika kipindi cha pili baada ya Neville kumnyang'anya mpira Ashley Cole na Kumkuta Laandon Donovan ambaye alipiga shuti kali lililompita Petr cech licha ya kulipangua na kutua wavuni.
Licha ya kupigana zaidi Chelsea walishindwa kubadilisha matokeo na hadi mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa 2-0,na kuwafanya wenyeji hao wa Stamford bridge wakishindwa kuondoka na Point tatu katika mechi nne mfululizo.
ARSENAL WAIBURUZA SUNDERLAND-
Thiery Henry ameipatia ushindi mwingine Arsenal hapo jana ilipocheza na Sunderland, na kuifanya timu kushinda kwa jumla ya magoli 2-1 baada ya kutanguliwa kwa goli moja na Sunderland katika uwanja wa Light.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilishuhudia Arsenal ikifanya mashambulizi machache kutokana na ulinzi imara wa Sunderland ingawa Arsenal walionekana kutawala kiasi kipindi hicho wakitumia nguvu za ziada kuwapita viungo na mabeki wa Sunderland.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Arsenal kufanya mashambulizi ingawa bado awakufua dafu kwa safu ya ulinzi ya sunderland. Badala yake Sunderland ndio walioanza kufanya mashaambulizi kupitia kwa Craig Gardner katika dakika za 61na 63 na kumfanya kipa wa Arsenal Wojciech kufanya kazi ya ziada.
hatiimaye Sunderland walipata goli lao dakika ya 70 baada ya makosa ya mlinzi wa Arsenal ambaye alipoteza mpira na kumfanya james Mc Clean kufunga goli hilo.
Baada ya goli hilo Arsenal nao walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 75 kupitia kwa machezaji Aaron Ramsey aliyepiga shuti lililogonga mwamba na kuingia golini.
Na mwishowe matokeo yakiwa yanaonekana kuwa sare Mchezaji anayeshika vichwa vya habari tangu arudi tena kwa muda Arsenal mkongwe thiery Henry alifunga Goli katika dakika ya 91 ya ambao ulikuwa ni muda wa nyongeza akiunganisha krosi ya Andrei Arshavin na kuifanya Arsenal kuibuka na Ushindi wa magoli 2-1.
Thiery Henry ambaye amerudi Arsenal kwa muda kutoka Marekani ambako anacheza soka kwa sasa amekuwa chachu na msaada wa ushindi wa Arsenal katika siku za hivi karibuni na pengine timu hiyo inauwezekano wa kufikiaria kumrudisha katika kikosi hicho cha Arsene wenger.
Saturday, February 11, 2012
NI GHANA VS MALI KUTAFUTA MSHINDI WA TATU AFCON.
Malabo-GUINEA YA IKWETA, Kikosi cha Mali
Ghana inaivaa Mali leo hii katika mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Mataifa ya Afrika bila wachezaji wake wanne tegemeo katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta Malabo.
Ghana imeingia katika nafasi hiyo baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Zambia na Mali walipoteza dhidi ya Ivory Coast katika nusu fainali.
Ghana ambao mafanikio yao yalikuwa juu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kutinga kuvunjika moyo baada ya kushindwa kufika Fainali katika michuano ya mwaka huu.
Mali kwa Upande wao wanajipongeza kwa kufikia hatua hiyo bila ya nyota wao wa kipindi kilichopita Fredrik Kanoute, Mamadou Diarra na Mamadou Sissoko, huku wakiegemea kupata faida ya kukosekana kwa wachezaji hao muhimu wa Ghana.
.
Hata hivyo mchezo huo unategemewa kuwa wa ushindani ambapo ghana wana kumbu kumbu ya Kuwafunga Mali magoli 2-0 katika hatua ya makundi.
ROONEY AIPAISHA MAN UNITED KILELENI.
Wayne Rooney amefunga mara mbili katika ushindi wa magoli 2-1 wa Manchester United dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Old Traford na kuisaidia timu yake hiyo kukwea kileleni mwa ligi hiyo.
katika Mechi hiyo ambayo ilishuhudia Manchester United wakitawala sehemu kubwa ya kipindi cha pili Rooney alifunga goli la kwanza katika dakika ya 47 baada ya kona na kuongeza goli la pili katika dakika ya 50 huku goli la liverpool likifungwa na Luis Suarez katika dakika ya 80 .
Katika mechi hiyo pia kulishudiwa muendelezo wa uhasimu kati ya Mchezaji Luis Suarez wa Liverpool na Patrice Evra wa manchester united Baada ya mchezaji huyo wa Liverpool kukataa kupeana mikono.
Kwa matokeo hayo Manchester United Imeshika Usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 58 mbele ya Manchester City wenye Pointi 57 wakiwa na mchezo mmoja mkononi wakati liverpool wao wanabaki na pointi zao 39 katika nafasi ya 7.
IRAN KUTANGAZA MAFANIKIO YAKE KATIKA MPANGO WAKE WA NYUKLIA.
Rais wa Iran Ahmadinejad amesema hivi karibuni nchi yake itatangaza mafanikio makubwa iliyoyapata katika mapango wake wa nyuklia.akihutubia makumi ya maelfuya watu katika sherehe za kutimiza miaka 79 ya mapinduzi ya nchi Ahmedinedjad amesema katika siku zijazo dunia itashuhudia kutangazwa kwa tangazo muhimu la mafanikio ya Iran katika mradi wake wa Nyuklia bila kufafanua zaidi.
Wafuasi wa Rais huyo wakiwa wamebeba bendera za Iran na picha za mwanamapinduzi na kiongozi mkuu wa kidini Bw Ayatollah ali Khamenei walipaza sauti zao kwa maneno ya kuzilaani Israel na Marekani.
Naye kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh aliyekuwa moja wa waalikwa katika sherehe hizo amesema kamwe Hamas hawataitambua Israael kama taifa, kiongozi huyo amesema ingawa wapinzani wao wanawataka kuacha upinzani dhidi ya Israel na kutambua uvamizi wa Israel kamwe hawatofanya hivyo kama wawakilishi wa Wapalestina.
Sherehe hizo zilikuwa za kukumbuka mapinduzi ya serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani ya rais Sha Mahammad Reza Pahlavi yaliyotokeaa Mnamo mwezi Februari 11, 1979 ambayo yalifuatiwa na Uundaji wa taifa la kiislamu chini ya Kiongozi Ayatollah Ruhollah Khomeini.
Thursday, February 9, 2012
IVORY COAST YAIFUATA ZAMBIA FAINALI, YAWATOA MALI.
Goli la nguvu na juhudi binafsi lake Mchezaji mahiri wa Ivory Coast anayeichezea Arsenal ya uingereza Yao Gervinho jana lilikuwa tosha kuwaingiza tembo kutoka magharibi ya Afrika katika fainali.
Gervinho ambaye tangu mwanzo wa mashindano haya kuanza alionekana kuwa katika chini ya kiwango jana aligeuka mwabi makali kwa goli lake hilo mahiri kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.
Ivory coast ambao walionekana kuwa moto tangu mwanzo wa mchezo kwa kuwakosa mali katika dakika ya 6 ya mchezo baada ya kichwa cha Didier Drogba kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Dakika kumi baadae baada ya shambulizi hili Salomon kalou alitoa pasi murua iliyomkuta Yaya Toure katika nafasi nzuri ya kufunga ingawa safu ya ulinzi ya Mali iliokoa shambulizi hilo.
Mwishowe katika dakika ya 45 Gervinho aliiandikia Goli timu yake baada ya juhudi binafsi ambapo alitumia kasi aliyonayo kusonga mpaka golini kutoka kati kati ya uwanja akitumia upande wa Kushoto na baadae kurudi kulia akiwa ndani ya eneo la kumi na nane na kufunga kwa mguu wa kulia.
katika kipindi cha pili hakukuwa na ushindani mkali kama kile cha kwanza ingawa timu zote mbili zilitengeneza nafasi ya kufunga, lakini bahati mbaya kwa Mali ambao hawakuweza kurudisha goli hilo mpaka mwisho wa mchezo.
Kwa matokea hayo mali watacheza na zambia siku ya Jumamosi kumtafuta mshindi wa 3, huku Ivory coast wakiwafuata Zambia katika fainali zitakazochezwa hapo jumapili ya tarehe 12 wezi huu Katika mji wa libreville.
MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA WAFIKIA KIKOMO-Katibu mkuu na mganga mkuu wasimamishwa kazi.
Mgomo wa Madaktari wa hospitali za umma nchini tanzania hatimaye umefikia kikomo leo hii huku kukishuhudiwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya ndugu. Blandina Nyoni na mganga Mkuu wa wa serikali bw. Deo Mtasiwa wakisimamishwa kazi kupisha Uchunguzi dhidi yao.
Hatua hiyo imekuja wakati waziri mkuu wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Pinda alipokutana na madaktari hao pamoja na wawakilishi wa wale wa mikoani kujadili suala hilo.
Katika kikao hicho serikali imekubali kuyashugulikia madai ya madaktari hao ambayo ni pamoja na Nyongeza ya mishahara, mazingira mazuri ya kazi na Marupurupu mengine ambay madaktari hao wanaidai Serikali.
Kwa Makubaliano hayo serikali na madaktari hao wamekubaliana kusitisha mgomo huo na Kurudi kazini kuanzia hapo kesho siku ya Ijumaa.
Mgomo huo umedumu kwa muda wa wiki tatu na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa kawaida ambao serikali za umma ndio kimbilio lao.
AFCON 2012- ZAMBIA YAIDUWAZA AFRIKA , YAITOA GHANA.
Kwa matokeo hayo Zambia wameingia fainali za michuano hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1994 walipofungwa na Nigeria Ambapo safari hii wanaenda kuktana na Ivory coast ambao jana wamewatoa mali kwa goli 1-0.
Ghana itabidi wajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi ikiwemo ile ya Penati iliyokoswa na Asamoah Gyan, huku nyota huyo na mwenzake john Mensah ambao ndio tegemeo la timu hiyo wakicheza chini ya kiwango.
Ghana walimaliza Mpira huo wakiwa watu 10 baada ya Mchezaji wake Derek boateng kupewa kadi nyekundu dakika sita kabla ya dakika 90 kumalizika bada ya kupokea kadi ya pili ya njano kutokana na faulo aliyoicheza.
Zambia wanaingia katika fainali hizo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya miaka 19 iliyopita huko gabon ambapo iliwapoteza wachezaji wake wote 25 baada ya ajali ya ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji hao.
Sunday, February 5, 2012
MANCHESTER YAIBANA CHELSEA NYUMBANI.
STAMFORD BRIDGE,
Manchester United leo wamejitutumua na kutoka nyuma ya magoli 3 hadi droo ya magoli 3-3 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Chelsea waliokuwa Uwanja wao wa nyumbani.
Chelsea walijikuta wakiongoza katika dak. 36 baada ya goli la kujifunga la Jonny Evans wa Manchester na baadae kufuatiwa na Magoli ya ya juan mata dak. 46 na David luiz dak. 51 na hivyo kuwa mbele kwa magoli 3-0.
hata hivyo wayne rooney alikuja kuvuruga furaha ya Chelsea baada ya kufunga penati zake mbili walizopata dakika ya 58 baada ya Sturidge kumchezea rafu Evra na dak. 69 baada ya Wellbeck kuguswa kidogo na Ivanovich na manmo dak. ya 84 javier harnandez aliifungia manchester United bao lake la tatu baada ya kupiga kichwa kilichomshinda Kipa Peter cech wa chelsea.
kwa matokeo hayo manchester City imeendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 57 ikifuatiwa na manchester united yenye point 55 na Totenham 49 huku chelsea Ikishika Nafasi ya Nne kwa kuwa na point 43.
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA- GHANA YAITOA TUNISIA, GABON HOI KWA MALI.
Wachezaji wa mali wakishangilia baada ya kuitoa Gabon kwa mikwaju ya Penati.
Andrew Ayew wa Ghana akichuana na mchezaji wa Tunisia
Mabingwa mara nne ya kombe la mataifa la Afrika timu ya Ghana leo wamefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuwafunga Tunisia jumla ya magoli 2-1 katika mchezo uliokuwa mkali na kushudia dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 kuisha timu hizo zikiwa katika sare ya 1-1.
Magoli ya ghana yalifungwa na John Mensah dak. 10 na Andrew Ayew Dk. 101 huku lile la Tunisia likifungwa na Saber Khelifa dak. 42.Katika mchezo huo Ghana ndio walioonekana kuutawala huku Tunisia wakiishia Kujilinda na kufanya mashambulizi machache langoni mwa Ghana.
Kwa matokeo hayo Ghana wanaenda nusu fainali kukutana na timu ya Zambia ambayo jana iliwatoa Sudan kwa jumla ya magoli 3-0.
katika Mchezo wa awali wa robo fainali Mali ilifanikiwa kuwabwaga wenyeji waliobakia na moja ya wababe wa michuano ya mwaka huu Gabon kwa changamoto za mikwaju ya Penati 5-4 baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1-1 katika dakika 90 za kawaida magoli yakifungwa na Erick Mouloungui wa Gabon dak. ya 55 na Chek diabate kwa upande wa mali daak. 84.
Ilipofika kipindi cha penati Mali walifunga penati zao zote lakini bahati mbaya kwa nyota wa Gabon Aubameyang ambaye shuti lake liliokolewa na kipa Diakate wa mali kabla ya Keita kufunga penati ya mwisho iliyoyafukia matumaini ya Gabon kusonga mbele katika michuano hiyo, kwa matokea hayo Mali inakwenda kukutana na Ivory coast ambayo jana pia iliwatoa wenyeji wengine wa michuano hiyo Guinea Bissau.
Saturday, February 4, 2012
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA- GUINEA NA SUDAN ZATUPWA NJE ZAMBIA NA IVORY COAST ZAPETA.
MALABO-GUINEA, Ivory coast imezima ndoto za moja ya wenyeji wa kombe la mataifa ya afrika mwaka 2012 Guinea bissau kusonga mbele katika nusu fainali baada ya Kuirarua kwa jumla ya mabao 3-0, magoli yakifungwa na Didier Drogba Katika dakika ya 36 na 69, pamoja na Yaya Toure dakika ya 81.
Ivory coast walistahili kushinda mechi hiyo hasa kutokana na kuonesha kiwango kizuri na kutawala mchezo tangu mwanzo hata hivyo wanapaswa kujilaumu kwa kukosa nafasi nyingi za wazi ikiwemo Penati iliyopigwa na Didier dgorgba na kuokolewa na kipa wa Guinea katika Dakika ya 29 na pamoja ile ya wilfred Borni dakika ya 93 alipopiga shuti lililopita sentimeta chache pembeni ya goli baada ya kubaki na kipa.
Kwa matokeo hayo wenyeji hao wameyaaga mashindano hayo na Ivory coast itamsubiri mshindi kati ya Gabon na mali katika robo fainali nyingine hapo jumapili.
katika robo fainali ya kwanza Zambia nao walikata tiketi ya Nusu fainali baada ya kuwafunga Sudan kwa jumla ya magoli 3-0, magoli ya zambia yakifungwa na Stoppila Sunzu dk 15, Chrios Katongo dk 66 na James Chamanga dk 86. Kwa matokeo hayo Zambia itamsubiri mshindi kati ya Tunisia na Ghana hapo kesho.
Friday, February 3, 2012
TAMKO LA MAKUBALIANO YA MKUTANO KATI YA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI NA ‘TASK FORCE’ YA MADAKTARI BINGWA WA MNH LATOLEWA.
Dar es Salaam -Tanzania, kamati ya jumuiya ya madaktari na Kikosi kazi cha Madaktari Bingwa wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili wamekutana na kufanya Mkutano kuhusu hali ya mgomo wa madaktari wa sekta ya umma hapa nchini hapo jana ambapo wametoa tamko lao rasmi kwa vyombo.
Tamko lao rasmi:
2. TUMEKUBALIANA KUWA NA TAARIFA YA UPOTOSHAJI JUU YA MALENGO YA TIMU HIYO YA MADAKTARI BINGWA, KIMSINGI LENGO LAO HASA ILIKUWA NI KUISHINIKIZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA HARAKA ILI KUNUSURU HALI YA AFYA NCHINI.
3. PIA TUMEKUBALIANA KUWA KUTOKANA NA HALI YA UZOROTAJI WA HUDUMA YA AFYA TUNATOA MWITO KWAMBA KAMATI KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MADAKTARI KUWA IPO TAYARI HATA LEO KUKAA NA SERIKALI MEZANI ILI KUFIKIA HITIMISHO YA MGOGORO HUU.
4. TUNGEPENDA SERIKALI KUACHA KUTOA VITISHO NA KUKAMATA NA KUWEKA RUMANDE BAADHI YA MADAKTARI HAPA NCHINI. KITENDO HICHO HAKITOI SULUHU YA TATIZO HUSIKA.
5. MWISHO SERIKALI ISIJARIBU KUKWEPA KUWASILIANA NA KAMATI SABABU KAMA KUNA NJIA YOYOTE YA KUFIKIA SULUHU YA TATIZO HILI NI KUPITIA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI.
Thursday, February 2, 2012
WATU 73 WAFARIKI KATIKA VURUGU ZA SOKA EGYPT
PORT SAID, EGYPT
Watu 73 wameripotiwa kufa na wengine 1,000 kujeruhiwa katika vurugu kubwa za mchezo wa soka kati ya mashabiki wa Timu ya Al ahli iliyokuwa ikicheza dhidi ya timu ya Al-Masry yenye maskani yake mjini humo. Vurugu hizo zimeibuka Mwisho wa mechi iliyoshuhudia timu ya Al-Masry Ikipata ushindi wa Magoli 3-1 dhidi ya wapinzani wao Al ahli.
Picha za televisheni zimeonesha mashabiki wa Timu ya Al-Masry Wakiingia Uwanjani na Kuwakimbiza Wachezaji wa Al ahli pamoja na mashabiki wao ambapo iliwalazimu kukimbilia kwenye chumba cha kubadilishia nguo hadi polisi walipokuja kuwaokoa na kuwatoa wakishirikiana na vikosi vya jeshi vilivyowasafirisha wachezji na majeruhi kwa helikopta. Shirikisho la mpira nchini humo limesogeza mbele baadhi ya mechi za ligi hiyo baada ya vurugu hizo huku Bunge likitarajiwa kukutan kesho kwa kikao cha dharura kujadili suala hilo.
Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Bw. Hosni Mubarak wametuhumiwa kuchochea vurugu hizo ingawa historia imeonesha uwepo wa matukio ya vurugu zinapokutana timu hizo, ingawa pia ukosefu wa Polisi umeonekana moja ya sababu za vurugu katika mechi za hivi karibuni nchini humo.
Mwanasheria mkuu wa Egypt ameagiza kufanyika uchunguzi mara moja juu ya tukio hilo huku naibu waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Hesham Sheiha akilitaja tukio hilo kuwa baya kabisa kupata kutokeaa katika Medani ya soka Nchini humo.
Wednesday, February 1, 2012
MITT ROMNEY ASHINDA FLORIDA.
FLORIDA, MAREKANI,
Gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney amepata ushindi katika kinyang'anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais kupitia chama cha Republican katika Jimbo la Florida siku ya Jumanne. Ushindi huo umemfanya Romney kuwa kinara wa kinyang'anyiro hicho akiwatupa wapinzani wake wa karibu Bw.Gingrich na Bw.Santorum.
Matokea ya kinyang'anyiro katika Jimbo hilo yameonesha Romney amejipatia 47% , Gingrich 32%, Santorum 13% na Paul akiambulia 7% ya kura zote.
Katika hotuba yake ya Ushindi Bw. Romney amepinga wazo kuwa kinyang;anyiro hicho kinakidhoofisha chama cha Republican :
"Kinyang'anyiro hicho hakitugawanyi bali kinatuandaa" alisema bw.Romney akiwa Tampa Florida.
Mgombea huyo badala yake aligeuza kibao kutoka kwa wagombea wenzake kwenda kwa rais Obama akisema rais huyo alichaguliwa kuongoza lakini amechagua kuongozwa kwa hiyo atoke nje ya njia kuwapisha wengine akitumia msemo wa manafilosofia maarufu Thomas paine aliyesema"Ongoza,Ongozwa au toka kabisa kwenye Njia"
Kwa matokeo hayo Romney ameshika nafasi ya kwanza,akifuatiwa na Gingrich alimaliza wa pili, huku Rick santorum akichukua nafasi ya tatu na Ron Paul ya nne.
Kwa upande wake Gingrich amesema maatokeo hayo yameongeza ushindani wa mwakilishi wa chama chao katika Uchaguzi ujao na akasisitiza kuendelea na kinyang;anyiro hicho.
"Tutaendelea kushindana kila sehemu na tutashinda na kurudi hapa Tampa kama wagombea wa Urais hapo mwezi wa nane" aliongea Gingrich kutoka aliongea makao yake makuu huko Orlando. Gingrich aliongeza kuwa ataonesha ni kwa jinsi gani "nguvu ya umma" itashinda "Fedha" katika kinyang'anyiro hicho.
Mgombea mwingine aliyeshika nafasi ya tau Bwana Santorum amesema ataendelea kupambana na kuwataka wagombea wenzake kujikita zaidi katika hoja muhimu badala ya kupakana matope.
kwa upande wake Paul pia amejipa moyo wa kuendelea ambapo katika hotuba yake aliyoitoa huko Nevada baada ya kumpigia simu Romney na kumpongeza alisema "Nimemwambia pia kuwa tutaonana Majimbo ya Caucus" Alisema Paul ambaye nguvu zake kwa sasa amezielekeza katika majimbo ya Nevada, Colorado na Maine ambayo yapo katika ratiba ya kupiga kura wiki chache zijazo.
Ushindi huo wa Romney unamfanya kuwa mgombea Pekee kuongoza mara mbili katika kinyang'anyiro hicho kufuatia ushindi wake huko New Hampshire's tarehe 10 Januari. ushindi huo umeonesha uwezo wa Romney kushindana huku kura nyingi za maoni zikionesha Romney anachagulika moja ya sababu zinazoaminika kuchangia ushindi huo wa Florida.